ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 17, 2010

Terry amjeruhi mlinzi wa Chelsea kwa gari


John Terry of Chelsea celebrates after scoring the opening goal during the Barclays Premier League match between Chelsea and Manchester United at Stamford Bridge on November 8, 2009 in London, England.  
Mlinzi katika uwanja wa klabu ya Chelsea amejeruhiwa baada ya gari la nahodha wa klabu hiyo John Terry kumgonga wakati Terry akiondoka uwanja wa Stamford Bridge.
Taarifa ya klabu imesema, alimgonga mlinzi huyo wakati akiendesha polepole akiwapita wapiga picha na mashabiki baada ya kutandikwa bao 1-0 na Inter Milan na kutolewa katika mashindano ya kuwania ubingwa wa vilabu vya Ulaya, usiku wa Jumanne.
Mlinzi huyo wa klabu alianguka na alichubuka vibaya mguuni.
Klabu ya Chelsea imesema Terry, wakati anaondoka alifahamu "alimgusa mtu" kwa gari yake lakini hakuwa na mawazo kama alimjeruhi mtu yeyote.
Msemaji wa Chelsea amesema: "Tunaweza kuthibitisha kulitokea ajali wakati John Terry akiondoka uwanja wa Stamford Bridge usiku wa Jumanne."

No comments: