Wabongo 200 kuula World Cup!
Former South African President Nelson Mandela addresses the Final Draw for the FIFA World Cup 2010 December 4, 2009 at the International Convention Centre in Cape Town, South Africa.Kampuni la vinywaji laini la Coca Cola litawapanddisha pipa wabongo 200 kushuhudia fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Afrika Kusini baadaye Juni.
Wabongo hao watatokana na promosheni maalum itakayojulikana kama 'Kwea Pipa na Ushinde' na watashuhudia mechi ya Brazil na Ureno mchezo utakaochezwa Juni 26 Durban, Afrika Kusini.
Washindi hao watakaokwenda Afrika Kusini, watagharamiwa kila kitu tiketi ya kwenda na kurudi, chakula, malazi pamoja na usafiri wa ndani.
Akieleza kwanini walichagua mchezo huo wa Brazil na Ureno, meneja fedha wa kampuni hiyo, Valence Pantaleo alisema ni kutokana na ushindani mkubwa uliopo kati ya timu hizo
No comments:
Post a Comment