ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, April 3, 2010

Mkuu wa Anglikana ashutumu kuwaingilia watoto


   
Kiongozi wa Kanisa la Anglikana duniani, Dr Rowan Williams, amesema Kanisa Katoliki nchini Ireland limepoteza "uaminifu wake wote" kutokana na jinsi lilivyoshughulikia suala la makasisi wanaodaiwa kuwaingilia kimwili watoto.
Dr Williams alisema matatizo ya kanisa hilo yaliathiri jamii kwa vile yalisababisha tafrani kubwa.
Akizungumza na BBC, alisema madai ya kuwaingilia kimwili watoto yaliwafanya maaskofu washindwe kuonekana hadharani.
Hii ni mara ya kwanza kwa Dr Williams kuzungumzia kashfa hii.
Kashfa hii imezusha utata kuhusu namna Papa Benedict alivyoshughulikia shutuma za watoto kuingiliwa kimwili na makasisi, kabla ya kuwa Papa wa kanisa Katoliki.
Lakini wafuasi wake wamesema Papa alitoa kanuni kadhaa za kuwalinda watoto.

No comments: