
Wayne Rooney alipowasili toka Munich
Mshambuliaji wa England Wayne Rooney anaweza kuwa katika hali nzuri wakati wa Kombe la Dunia baada ya klabu yake ya Manchester United kueleza ameumia "kidogo tu mfupa" wa kiwiko cha mguu.
Taarifa iliyotolewa na klabu imesema: "Tunafuraha kuwaarifu Wayne hakuvunjika mfupa wowote wa kiwiko chake cha mguu. Kipimo kimeonesha ni jeraha dogo tu."
Bado haijafahamika ni mechi ngapi atakosa kuichezea Manchester United.
Meneja wake Sir Alex Ferguson atatoa maelezo zaidi juu ya hali ya Rooney na maendeleo ya hali yake siku ya Ijumaa asubuhi.
Mshambuliaji huyo ambaye kiwango chake cha kufunga mabao kimepanda msimu huu na tegemo kubwa la England katika Kombe la Dunia aliumia wakati wa mchezo wa kwanza wa robo fainali dhidi ya Bayern Munich siku ya Jumanne. Kwa vyovyote hataweza kucheza mchezo wa Jumamosi wa Ligi dhdi ya Chelsea.
Madaktari wamesema aina ya jeraha la Rooney linaweza kumlazimisha mchezaji kutocheza kwa kwa wiki tatu au nne na atamudu kucheza Kombe la Dunia.
No comments:
Post a Comment