ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 28, 2010

CCM wajipanga kumwokoa JK

Jakaya Mrisho Kikwete
Waandishi Wetu
SIKU moja baada ya Chadema kutangaza nia ya kumwekea pingamizi mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete, chama hicho tawala kimesema kuwa kinajipanga kumwokoa mgombea wake dhidi ya hoja za kutaka mgombea huyo aondolewe mapema.
Juzi, Chadema ilitangaza nia ya kuwasilisha pingamizi kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na kwamba ilitaka jana kumwekea pingamizi Kikwete kwa kuwa amekiuka sheria ya gharama za uchaguzi kwa kutangaza nyongeza ya mishahara ya wafanyakazi wa sekta ya umma kwenye mikutano ya kampeni.
Kikwete alishaeleza mapema kuwa serikali haiwezi kutekeleza mapendekezo ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) la kutaka kima cha chini cha wafanyakazi wa sekta ya umma kuwa Sh315,000 na hata shirikisho hilo liliposhusha madaio yake hadi Sh260,000, serikali ilisema haina uwezo huo.
Lakini katika siku za karibuni ilibainika kuwa mishahara ya wafanyakazi wa serikali imepanda kwa asilimia kubwa kiasi cha kima cha chini kufikia karibu "pendekezo la pili la Tucta", na Kikwete amekuwa akieleza hayo kwenye kampeni zake kama moja ya hatua zinazoonyesha serikali inawajali wafanyakazi.FULL STORY

No comments: