
Mgombea Urais wa chama cha CHADEMA,Willbrod Slaa,akizungumza leo jioni wakati wa uzinduzi wa kampeni na Ilani ya chama hicho,mbele ya maelfu ya watu waliofika kushuhudia uzinduzi huo katika viwanja vya Jangwani.Slaa alisema,akipewa ridhaa ya kuongoza Nchi hii,basi atahakikisha ndani ya siku 100 za kwanza anafanyia marekebisho makubwa KATIBA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,na pia kubadirisha mfumo wa Elimu Nchini.

Mgombea Urais chama cha CHADEMA,Mh:Willbrod Slaa,akimtambulisha mkewe mbele ya maelfu ya watu kwenye uzinduzi huo wa kampeni na Ilani ya chama hicho jioni ya leo katika viwanja vya Jangwani

Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Freeman Mbowe,akimkabidhi vitabu vya Ilani ya chama hicho kwa mgombea Urais wa chama,Mh:Willbrod Slaa leo jioni katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar mara baada ya uzinduzi wa kampeni.

Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Freeman Mbowe akionyesha vitabu vya Ilani ya chama hicho,mara baada ya kuizindua leo Jijini Dar katika viwanja vya Jangwani.

Wananchi wakionyesha kuunga mkono baadhi ya mambo yaliokua yakizungumziwa kwenye uzinduzi wa kampeni na Ilani ya chama hicho leo jioni katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar

Wananchi wakishangilia kwa nguvu zote

Mgombea ubunge kwa tiketi ya chama cha CHADEMA,jimbo la Kawe,Halima Mdee,akipitisha bakuri la kuomba msaada kutoka kwa watu mbali mbali waliofika viwanjani hapo,fedha hizo ambapo ilielezwa kuwa zitatumika kwenye mbio za kampeni ambazo wamezindua leo na wanatarajia kuzianza hivi karibuni Nchi nzima

Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Freeman Mbowe,akijaribu kuwatuliza baadhi ya wananchi kuwa wawe watulivu,hakuna kitakacho haribika,Mbowe ilibidi aingilie kati baada ya kubaini shirika la utangazaji la TBC 1,kukatisha matangazo ya uzinduzi wa kampeni na Ilani ya chama hicho,yaliyokua yakirushwa LIVE na hata wananchi wenye hasira kuthubutu kutaka kumpiga mmoja wa watangazaji wa kituo hicho na baadae TBC1 kuamriwa waondoke uwanjani hapo kwa usalama wao.

Mtangazaji wa shirika la utangazaji TBC1,Marin Hassan Marin,akiombwa aingie kwenye gari na aondoke eneo la tukio kutokana na baadhi ya wananchi kutofurahishwa na tukio la kukatisha ghafla kwa matangazo hayo yaliyokua yakirushwa LIVE na shirika hilo(picha kwa hisani ya JIACHIE)
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake