Saturday, August 7, 2010

Chuji, Humud ni ‘bhita’ Stars

Abdulhalim Humud
Na Wilbert Molandi
KUREJEA kwa kiungo wa Athumani Idd ‘Chuji’ kwenye timu ya Taifa Taifa Stars kumezua upinzani mkali dhidi ya Abdulhalim Humud kwenye kikosi hicho kinachoendelelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Karume jijini.

Vita hiyo ya namba ilianza juzi wakati Kocha Jan Poulsen raia wa Denmark alipoanza kibarua chake cha kuinoa Stars kwa kupanga vikosi viwili vyenye ushindani akiwa na lengo la kusaka kikosi chake cha kwanza.

Humud alikuwa wa kwanza kushuka kwenye basi la timu hiyo majira ya saa 9:44 alasiri akifuatiwa na beki wa pembeni Stephene Mwasika ambaye ni mchezaji wa kwanza kukanyaga uwanja huo wenye nyasi za bandia.

Timu hiyo ilianza mazoezi saa 9:47 kwa kukimbia mbio fupi na kunyoosha viungo, ikifuatia na kuruka koni pamoja na kupigiana pasi fupi na mipira mirefu, tukio lililochukua dakika kumi ili kuweka mwili fiti.

Baada ya kumaliza mazoezi hayo kocha huyo aliandaa vikosi viwili kwa kila mchezaji kumpanga nafasi yake anayocheza ambapo katikati ya uwanja alikuwa yupo Kocha Msaidizi Sylvester Marsh huku Poulsen akiwa pembeni kuangalia kiwango cha kila mchezaji.
Athumani Idd Chuji
Wakati mazoezi hayo yanaendelea Chuji na Humud walionyesha upinzani mkubwa kwa kila mmoja kutaka kuonyesha kiwango baada ya kuwapanga kila mmoja namba sita katika pande tofauti.

Chuji alimudu kupiga pasi 52 kati ya hizo tatu alipoteza na moja kuleta madhara kwenye lango lao, baada ya kumpigia pasi fupi beki Agrey Moris na winga Mrisho Ngassa kuunasa na kumfunga kipa Shabani Kado.

Humud alipiga pasi 19 alipoteza pasi moja pia alishindwa kupiga mashuti ya kulenga goli badala yake kupaisha mipira mitatu, Kiggi Makasi anaongozana na Ngassa kwa kuwa wachezaji wa kwanza kufunga mabao chini ya kocha mpya.

Poulsen lisema anahitaji muda zaidi katika kukiandaa kikosi hicho ambapo anatumia mfumo wa 4-3-3 na 4-5-1.


HABARI KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake