Wednesday, August 11, 2010

CLOUDS TV WAUNGANA NA MTV BASE

Usiku huu, ndani ya ukumbi wa Much More uliyopo katika jengo la Club Billicanas, umefanyika uzinduzi rasmi wa ushirikiano kati ya Clouds TV na televisheni ya Kimarekani MTV Base. katika ushirikiano huo, Clouds TV itakuwa ikirusha baadhi ya vipindi vya MTV Base kwa saa kadhaa kila siku jioni kuanzia saa 12. Pichani ni Mkurugenzi wa Clouds Entertainment Jose Kusaga (kulia) akitoa shukrani zake kwa MTV Base kupitia mwakilishi wao Mr. Paul
baadhi ya wadau waliohudhuria wakifuatilia kwenye TV uzinduzi huo.
wawakilishi wa MTV Africa, Seven (kushoto) na VJ Vanessa
wadau na wageni waalikwa, Afisa Uhusiano wa Serengeti Breweries Teddy Mapunda, akiwa na laaziz wake
nyota wa Bongo Juma Nature akiwa na Madam Rita ndani ya Much More usiku huu.
Msanii Diamond 'mzee wa mbagala' akiwa na kampani yake
wadau wa masuala ya ubunifu wa mavazi..Fideline akiwa na Mbunifu mitindo ya Mvazi, Ally Remtulla
Kiongozi wa Clouds TV, Ruge (kulia) akiteta jambo na Programme Manager wa Clouds TV.

PICHA: Abdallah Mrisho/GPL

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake