Sunday, August 15, 2010

H.baba kutoka na filamu ya ‘Promota


H.baba kutoka na filamu ya ‘Promota’

Na Andrew Chale
MSANII mahiri Hamis Ramadhan Baba “H.Baba’ yupo katika hatua ya mwisho kukamilisha filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Promota’.
H.baba alisema hayo mapema leo... alipokua akiojiwa na redio mmoja  nchini ..(TBC1) na kusema kua muda mwingi alikua akifanya muziki huku akijushughulisha na filamu fani ambayo alianza nayo muda mrefu.
“Filamu  yangu ya ‘Promota’ ni kali na itatishia soko la filamu nchini kutokana na mambo yaliyomo ndani ya filamu hiyo’ alisema H.baba.
Filamu hiyo inaongozwa chini ya  mtunzi na  mwalimu wa sanaa za maigizo na filamu nchini, July Tax, ambaye pia alimfundisha sanaa H.baba tokea akiwa na miaka minne katika kundi la Saladin.
Akiongelea zaidi juu ya filamu hiyo, H.baba alisema kua itakua na matukio mengi yakiwemo ya ‘Action’ ilikuweza kumvutia mtazamaji na kuongeza radha kwa wadau.
“Mimi ni mtaalamu wa filamu za ‘action’ hivyo nimejaribu kila aina ya uwezo wangu kuvaa uhusika, naomba wadau waisuburi kuona mambo makubwa, mimi sibahatishi nafanya kweli kama ninavyofanya katika muzuki na mpira wa miguu’ alisema H.baba.
Aidha, alidai kua amegundua sanaa ya filamu inalipa,  hivyo ameamua kujakitofauti na kuzidisha ujuzi zaidi.
Mpaka sasa ‘H- Baba’ ameweza kuingiza albamu tati sokono ana vipaji zaidi ya vitatu kikiwemo cha mpira wa miguu, kuimba na maigizo. Huku filamu alizoigza ndanii ya kundi lake la Saladini ni pamoja na ‘Mtemi’.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake