
Kwanza hebu tuangalie kutojiamini maana yake nini?
Kutojiamini hutokana na mtu kufanya kitu pasipo kuwa na uhakika kama upo sahihi hata kama yupo sahihi, hii hupelekea hata kile ulichokuwa ukikifanya kwa ufasaha kuona kama unakosea.
Na kwa nini mtu anashindwa kujiamini?
Mambo yanayomfanya mtu ashindwe kujiamini, hutokana na hofu moyoni inayopelekea aone kama anakosea hata kama yupo sahihi. Hii hupelekea kushindwa afanye nini matokeo yake uharibu kabisa.
Leo nataka tuzungumzie mtu kujishindwa kujiamini katika mapenzi, kutokujiamini katika mapenzi hukufanya ushindwe kufanya mapenzi kwa asilimia mia. Hii imesababisha mahusiano mengi kulega au hata kuvunjika kutokana wapenzi wengi kushindwa kuwaridhisha wenza wao.
Ni kwa nini mtu hupoteza kujiamini?
Watu wengi hupoteza kujiamini kutokana na mawazo yao kupingana na uhalisia. Kwa kuamini kila alichonacho au anachokifanya kwake ni bahati au hakutegemea kukipata au kukifanya.
Kumekuwa na tatizo la mtu kuamini mtu fulani ni wa hadhi ya watu fulani na si ‘saizi’ yake.
Na ikitokea siku yule mtu umempata pengine mzuri sana au mtanashati mwenye fedha. Ukiwa naye badala ya kumpa kile mwenzio alichokitaka kwako, unatumia muda mwingi kupingana na mawazo yako katika uhalisia wa tukio lile.
Hata mkiwa ndani ya mapenzi muda mwingi unautumia kujiuliza ni kweli au ndoto, ukiwa katika hali hii utajikuta ukimuogopa mwenzako kwa kuamini huenda utakachokifanya kitamuudhi au utakikosea. Mwisho wa siku hukumfurahisha aibu inachukua sehemu kubwa.
Nini cha kufanya:
Siku zote unatakiwa ujiamini kwa lolote unalofanya lazima utalifanya kwa asilimia kubwa, kama uzuri au fedha ni zake, lakini penzi linabakia palepale halibebwi na uzuri wa mtu wala fedha bali juhudi zako binafsi.
Ukiwa na mwanamke au mwanaume ambaye hukumtegemea siku moja kulala kitanda kimoja mtendee haki kwa vile mwanamke yeyote ni nyama isiyo na mfupa kwa mwanaume aliyefananishwa na kisu kikali.
Hata kwa wanawake vile vile, usimuogope mwanaume kwa fedha zake kama amekutaka kimapenzi kuna kitu anakitaka kwako si kumshangaa au kujiuliza hivi kweli mimi niko naye. Kufanya hivyo ni kupoteza ladha ya mapenzi. Jiamini muonyeshe kwamba unaweza usichojua si vibaya kuuliza.
Jiamini kuwa na wewe unastahili vitu vizuri au vitamu, hakuna aliyeumbwa kupata vibaya, kila kiumbe kina haki sawa katika mapenzi.
Tumetofautiana katika madaraja ya uwezo wa fedha na uzuri. Lakini penzi ni kitu cha bure mtaji wake kujituma na kujiamini, hakika mpenzio atafaidi penzi lako.
Na Ally
Mbetu Simu:
+225 713 646500
E-mail: ambedkt@yahoo.com
Kwa hayo machache tukutane wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment