Anne Kilango, mpambanaji wa ufisadi ambaye ameng'ara katika uchaguzi wa kura za maoni ndani ya CCM
Waandishi Wetu
JABALI la siasa nchini, John Malecela, maarufu kama tingatinga yuko katika hali mbaya kutokana na kubanwa mbavu kwenye kura za maoni, huku baadhi ya mawaziri wakiwa katika hatihati ya kupoteza ubunge, kwa mujibu wa matokeo ya awali ya kura za maoni ndani ya CCM.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Diodorus Kamala, na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati walikuwa kwenye hali mbaya baada ya matokeo ya awali ya kura za maoni kutangazwa.
Lakini Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe walikuwa miongoni mwa mawaziri waliokuwa wakielekea kushinda, sambamba na naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi huku ushindi wa naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera ukiamsha vurugu wilayani Korogwe.
Mbali na mawaziri, wabunge kadhaa ambao walikuwa vinara kwenye Bunge la Tisa wanaweza kuwa wamefunguliwa mlango wa kwenda nje ya chombo hicho cha kutunga sheria.
Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii, mbunge wa Bumbuli, William Shelukindo, Mudhihir Mohamed Mudhihir (Mchinga), Tatu Ntimizi (Igalula), Siraju Kaboyonga (Tabora Mjini), Wilson Masilingi (Muleba Kusini) na mbunge wa Vunjo, Aloyce Kimaro wakiwa kwenye hali ngumu ambayo inaweza kuwafanya wasirudi bungeni.
Lakini wabunge wengine walio kwenye orodha ya wapambanaji, Harrison Mwakyembe (Kyela), Anne Killango (Same Mashariki), mbunge wa Ilala, Mussa Hassan Zungu na Jenister Mhagama (Peramiho) walikuwa wakielekea kuibuka na ushindi na kurejea kwenye chombo cha kutunga sheria.
Wagombea wapya ambao wanaonekana kuelekea kuingia bungeni ni pamoja na katibu mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka (TFF), Frederick Mwakalebela ambaye anaelekea kumuangusha Monica Mbega (Iringa Mjini), Hussein Bashe ambaye anaelekea kumshinda Selelii (Nzega), Donald Max ambaye anaelekea kumshinda Ernest Mabina wa Geita na Januari Makamba, ambaye alikuwa anaelekea kumshinda Shelukindo jimbo la Bumburi.KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake