Magari na wafanyakazi wa kikosi cha Zima moto wakiwa katika harakati za kuzima moto huo.
Nyumba moja iliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam inayomilikiwa na Bi. Hadija, imeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa kwani mali zote zilizokuwemo zimeungua. Moto huo ulitokea siku ya Ijumaa Agost 27, na kusababisha hasara inayokadiriwa kufikia shilingi Milioni 3. Akizungumza kwa masikitiko katika eneo la tukio, Hadija alisema moto huo ulisababishwa na mshumaa uliowashwa na mtoto wa mpangaji wake ambao uliangukia juu ya kitanda ambapo godoro lilishika moto uliosababisha nyumba hiyo kuteketea kabisa.
Moshi ukitanda wakati nyumba hiyo iliyoko Kariakoo ikiungua.
Wananchi mbalimbali wakishuhudia tukio hilo la kusikitisha.
Askari wa Zimamoto wakiendelea na zoezi la kuzima moto huo.
HABARI NA PICHA BY SHAKOOR JONGO / GPL
HABARI NA PICHA BY SHAKOOR JONGO / GPL
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake