
Chatu Albino anayefanana na huyo aliyekamatwa nchini Italia.
POLISI nchini Italia wamemkamata chatu asiye wa kawaida ambaye ni albino aliyekuwa anatumiwa na wauza madawa ya kulevya ili kulinda mizigo ya madawa hayo.Walimkamata mnyama huyo mwenye urefu wa mita tatu baada ya kutumia ujanja wa kumtupia kuku. Pia watu 12 wanaohusika na madawa hayo walikamatwa katika msako uliofanyika Jumanne usiku wiki hii.
Polisi wanaona ‘chatu mlinzi’ huyo alikuwa anatumiwa aidha kuwaogopesha watu wenye kuendesha msako dhidi ya madawa ya kulevya au kuwaogofya watumiaji wa madawa hayo (mateja) ambao walikuwa wanadaiwa fedha na kundi hilo, na ndiyo maana waliomweka humo walihakikisha anakuwa na njaa kali ili awe mkali zaidi.
Msako huo waliufanya wakiwa wamedokezwa kwamba wangekutana na ‘mnyama’, na huenda ndiyo sababu iliyowafanya kumchukua kuku na kwenda naye.
Nyoka huyo amepelekwa kwenye bustani ya wanyama jijini Rome, na watu 12 waliokamatwa wamefunguliwa mashitaka ya kuwa na kiumbe huyo anayelindwa kisheria na kwa kufanya biashara ya kuuza madawa hayo ya kulevya aina ya cocaine.
CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake