Tuesday, August 31, 2010

Tendwa atabiri viti 100 vya ubunge kwenda upinzani

Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu ofisi yake kupokea rasmi malalamiko ya chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema yanayodai mgombea urais kupitia CCM kukiuka sheria ya ghalama za uchaguzi . Picha na Said Powa
Na Ramadhan Semtawa

WAKATI joto la uchaguzi likizidi kupanda, Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tenda ametabiri kuwa vya vya upinzani vinaweza kupata viti 80 hadi 100 kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano kama watacheza karata zao vizuri. Msajili ametoa kauli hiyo wakati upinzani ukionekana kuzidi kukua baada ya wabunge kadhaa wa chama tawala kuhamia vyama vya upinzani kutokana na kutokubaliana na mchakato wa kura za maoni na matokeo yake, huku baadhi ya vyama vikijiimarisha kwenye majimbo kwa kuweka wanachama wenye nguvu, wakiwemo viongozi wao wakuu.

Wanachama wengi walioihama CCM na kuhamia upinzani wamesimamishwa kwenye majimbo waliyokuwa wakiyashikilia zamani kupambana na chama tawala, wakati Chadema na TLP zikisimamisha wenyeviti wao kugombea ubunge.

Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana kuhusu mwelekeo wa uchaguzi huo, Tendwa  alisema mtazamo wake unatokana na sababu kuu nne ambazo anaamini zitaongeza idadi ya wapinzani bungeni kama wakicheza vizuri karata zao.

"Wapinzani wanaweza kupata viti kati ya 80 hadi 100 kama wataweza kujipanga vema. Temperature (joto) ya kisiasa iko juu sana kwa sasa," alisema msajili huyo.FULL STORY

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake