
Getrude Mongella
Na Elvan Stambuli WAKATI kampeni zikiwa zinaendelea kupamba moto, baadhi ya wagombea wameng’ang’ania kuwawekea pingamizi wenzao wanaopambana nao katika majimbo ya uchaguzi.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa majimbo kadhaa wagombea wanaangaliana kwa jicho pembe huku wengine wakisisitiza kuwa wanataka waliowawekea pingamizi wang’olewe na wasimamizi wa uchaguzi.
Christopher Ole Sendeka
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amewekewa pingamizi na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Faya Kimbita ambaye anadai kuwa mgombea huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa taifa wa chama chake anadaiwa kuwa amekwepa kulipa kodi na serikali.Kimbita alidai katika barua yake ya pingamizi kuwa Mbowe alikwepa kulipa kodi kupitia Hoteli yake ya Aishi kuanzia Desemba 2009 hadi Novemba 2009 na kwamba kitendo hicho kinamuondolea sifa ya kuwa kiongozi.
William Lukuvi
Naye Getrude Mongella wa Jimbo la Ukerewe (CCM) amemuwekea pingamizi mgombea mwenzake, Salvatory Machemli wa Chadema kwa madai ya kukiuka taratibu za ugombeaji ubunge jimboni humo. Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo, Dk. Leopord Masale amethibitisha kupata pingamizi hilo.Habari kutoka Mbeya zinasema mgombea wa CCM wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Mchungaji Luckon Mwanjala amewawekea pingamizi wagombea wenzake, Sambwee Shitambala wa Chadema kutokana na fomu zake kuwa na kasoro na Ndele Mboma wa UDP kutokana na fomu alizojaza kutokuwa na anuani kamili.
Celine Kombani
Kutoka Jimbo la Bahi Dodoma, habari zinasema Badwel Omar wa CCM kawekea pingamizi wagombea wote anaopambana nao ambao ni), Melkzedech Lesaka wa SAU na Eva Abel Kaka wa CUF wakidaiwa kughushi sahihi za mawakala na William Kimboya wa UPDP anadaiwa fomu zake alizojaza zina kasoro kubwa.Wakati huo huo, mgombea wa CCM wa Jimbo la Bariadi Kaskazini, Martine Makondo ameahidi kuwa ni lazima safari hii wamng’oe Mwenyekiti wa UDP, John Momose Cheyo aliyekalia kiti hicho kwa miaka 14.
Mark Mwandosya
“Umri wake ni mkubwa safari hii sisi wana CCM tumeapa kuwa ni lazima tumng’oe,” alisema Makondo, madai ambayo yalipingwa na wapambe wa Cheyo akiwemo Mzee Maduhu aliyesema bado wanamhitaji kuwaongoza.Wakati kampeni zikiwa zimepamba moto kuwashawishi wapiga kura wawachague waliojitokeza, baadhi ya wagombea kupitia tiketi ya CCM wamepita bila kupingwa hali inayoashiria ‘asubuhi njema’ kwa chama hicho.
Anna Tibaijuka
Wagombea ambao walipita bila kupingwa na majimbo yao katika mabano ni Januari Makamba (Bumbuli), Deo Filikunjombe (Ludewa), Gregory Tau (Mpwapwa), Anna Makinda (Njombe kusini), na William Lukuvi (Isimani), William Ngeleja (Sengerema), Lawrence Masha (Nyamagana), Mohamed Dewji (Singida mjini) na Nimrodi Mkono (Musoma mjini).Wengine ni Celina Kombani (Ulanga mashariki), Christopher Ole sendeka (Simanjiro), na Profesa Anna Tibaijuka (Muleba kusini).
Wabunge wateule wengine ni Philipo Mulugo ( Songwe), Profesa Mark Mwandosya (Mwakaleli), Bernad Membe (Mtama) na Job Ndugai (Kongwa).
Katika hatua nyingine, wakati Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) imeshapuliza kipyenga cha kuanza kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 Agosti 20, mwaka huu, wenzao, Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar, (ZEC) imesema zoezi hilo kwa wagombea urais, uwakilishi na udiwani litaanza Septemba 10, mwaka huu.
Taarifa iliyopatikana kutoka katika tume hiyo imesema kampeni kwa wagombea hao wote zitamalizika Oktoba 31, siku moja kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31, 2010.
Vyama vyagongana
Wakati huo huo, Chama cha APPT Maendeleo na CUF viligongana katika viwanja vya Zakheem mwishoni mwa wiki baada ya kila kimoja kudai kilikuwa na haki ya kutumia uwanja huo.
Haikuweza kufahamika mara moja kilichosababisha kuingiliana kwa ratiba kwa vyama hivyo hali iliyosababisha kuwepo kwa mikutano miwili katika uwanja huo.
Hata hivyo, mgombea Urais wa APPT maendeleo, Peter Mziray alidai Cuf waliingilia ratiba hiyo kwa kuwa chama chake kilikuwa na kibali cha kufanya uzinduzi katika uwanja huo.
Hata hivyo, Mziray aliwahutubia wananchi waliofika kumsikiliza kwa kuwaahidi kuwa akichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atawakomboa katika umaskini.
“Ninaahidi nitawawezesha katika sekta ya kijamii ili kuwakomboa katika umaskini,” alisema Mziray ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho na aliwataka waliohudhuria kufikisha ujumbe huo kwa watu wasiofika kumsikiliza.
Wapiga kura wasinywe pombe
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kilimanjaro, Vicky Nsilo Swai amewataka wapiga kura kwenda kwenye mikutano na siku ya kupiga kura kutokunywa pombe.
Akizindua kampeni za uchaguzi kimkoa hafla iliyofanyika katika Jimbo la Siha, Swai alisema wakati wote wa kampeni wawe makini kusikiliza sera.
Aidha, aliwataka waliokuwa wakiwania kuchaguliwa ubunge katika kura za maoni kuvunja makundi.
Hivi sasa katika Jimbo la Moshi mjini, baadhi ya wanachama wanalalamikia kuenguliwa kwa mgombea waliyemchagua Athuman Ramole na kuwekwa Justine Salakana.
“Sisi kama wanachama ni lazima tulalamike kwa sababu kama ni hivyo hakukuwa na haja ya kutusumbua kufanya uchaguzi. Bora hata angewekwa mshindi wa pili, Thomas Ngawaiya, lakini wamemchukua mtu wa tatu, hii si haki,” alilalamika Massawe Manka aliyejitambulisha kama mkereketwa mkubwa na CCM.
Ngawaiya ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa Mkoa wa Kilimanjaro, alipohojiwa na mwandishi wetu kuhusu sakata hilo alisema hana kinyongo na atampigia debe mgombea aliyeteuliwa na chama.
CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS





No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake