
JAJI mstaafu wa Mahakama ya Rufaa nchini, Lameck Mfalila
JAJI mstaafu wa Mahakama ya Rufaa nchini, Lameck Mfalila, amewataka Watanzania kuchagua mgombea aliyethubutu kusema; "atasomesha wanafunzi na kutoa huduma ya afya bure." Akitetea msimamo huo, Jaji Mfalila alisema:"Huyu ni shujaa, sio ghilba bali amethubutu kusema anaweza kufanya mabadiliko hayo, mchagueni."
Katika mkutano wa wanaharakati kuhusiana na Uchaguzi Mkuu jijini Dar es Salaam jana, Jaji Mfalila alitoa sifa kwa mgombea mmojawapo wa urais kutoka kambi ya upinzani ambaye ameweka wazi kwamba akiingia Ikulu, elimu na afya zitatolewa bure.
“Kuna mgombea mmoja kutoka kwenye vyama vya upinzani, naona anaitia changamoto serikali, yeye alithubutu kusema ikiwa atachaguliwa kuingia Ikulu, atasomesha wanafunzi na kutoa huduma ya afya bure, huyu ni shujaa, sio ghilba bali amethubutu kusema anaweza kufanya mabadiliko hayo, mchagueni,” alisisitiza.FULL STORY
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake