
Meneja Mkuu wa Ulinzi wa jengo hilo Bw. Abuubakar Bashir (kulia) akipewa pole na msamaria mwema leo asubuhi katika ofisi ya mauzo ya sehemu iliyoungua.
Jengo la Quality Plaza ambalo linamilikiwa na Mfadhili Mkuu wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji lililoko barabara ya Nyerere, jijini Dar es Salaam, Alhamis iliyopita lilishika moto na baadhi ya sehemu kuteketea. Moto huo ulianzia upande wa benki Standard iliyopo kwenye jengo hilo na hatimaye kusambaa sehemu mbalimbali za jengo hilo. Moto huo ulianza kuwaka majira ya saa 4 usiku, kwa mujibu wa Meneja Usalama wa jengo amesema mpaka sasa kiasi cha hasara iliyopatikana bado hakifahamika na uchunguzi dhidi ya tukio hilo unaendelea.2 Muonekanao wa jengo unavyooneka kwa nje.
Baadhi ya vifaa vilivyotumika katika kuzima moto huo.
Hapa ni sehemu ya kutunzuia pesa ‘safe’ ambayo haikuungua kwa mujibu wa meneja usalama.
PICHA: HARUNI SANCHAWA / GPL.



No comments:
Post a Comment