
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Jakaya Kikwete ,akiwa ameketi chini ardhini ili kumsikiliza Mama Sara Mageni mkazi wa Wilaya ya Makete, wakati mgombea huyo alipowasili kuhutubia mkutano wa kampeni. Sara alikuwa akitoa shukrani zake kwa Rais Kikwete baada ya kumnunulia Bajaj ili kurahisisha shughuli zake, alipotembelea wilaya hiyo mwaka jana
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete alitumia staili ya aina yake kuomba kura wakati alipolazimika kuketi ardhini ili kumsikiliza mwananchi wakati akiwa kwenye moja ya mikutano ya kampeni za kuomba kura kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31.
Mbali na tukio hilo, kabla ya kupanda jukwaani mjini Ludewa wilayani Mbalali, Kikwete alikuwa akizungumza na simu na baada ya kumaliza aliwaambia wananchi kuwa alikuwa akizungumza na balozi wa Marekani nchini Tanzania na kwamba balozi huyo amemueleza kuwa Rais Barack Obama ameahidi kuwa serikali yake itaendelea kutoa misaada kwa Tanzania.
Watu wengi hawakuamini macho yao wakati Kikwete alipoanza kukaa chini kwa ajili ya kumsikiliza mwananchi huyo, Sara Mageni kwenye mkutano wake uliofanyika kwenye Uwanja wa Mabehewa wilayani Makete ambako wakati huu wa majira ya kipupwe vumbi limeshamiri.
Sara, ambaye ni mlemavu wa miguu, alikuwa akitoa shukrani zake kwa Kikwete ambaye alimnunulia pikipiki ya matairi matatu aina ya Bajaj ili kurahisisha shughuli zake wakati mwenyekiti huyo wa CCM alipotembelea wilaya hiyo mwaka jana.FULL STORY
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake