
Jumuiya ya WaTanzania waishio New York na vitongoji vyake(NYMTC) tukishirikiana na jumuiya ya waislam ya Washington Dc kwa pamoja na offisi za balozi wetu za Washington DC,tunatoa taarifa ya mazishi ya Ndugu yetu Amour Hemed Ally(Abraham Allen)yatakayofanyika siku ya alkhamis 09/23/2010 pale Harrisburg PA,saa 7:00(1:00PM) baada ya sala ya adhuhuri.Tafadhali heshimu wakati makaburi yanafungwa baada ya hapo.
Tunawaomba wale wote walioahidi ama watakaopenda kutoa michango,bado inahitajika hivyo wawasiliane na wahusika ili tuweze kumsitiri mwenzetu.michango iliyokusanywa bado haijatosheleza kukamilisha shughuli hii.
Tunawasisitiza wale wote watakaokuwa na nafasi wajitokeze kwa wingi ili kwa pamoja tuweze kuusindikiza mwili wa ndugu yetu.
Wasiliana na wafutao kwa taratibu za safari:
kutoka Washington DC
Yacob Kinyemi;202-629-7841
New York:Shabani Mseba:347-712-8539
MAJOR WINFIELD FUNERAL HOME
704 NORTH FRONT STREET
STEELTON,PA,17113
TEL;717-939-3342
SHUKRAN,
HAJJI KHAMIS
INTERIM CHAIRMAN
NEW YORK METRO TANZANIANS COMMUNITY.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake