Saturday, September 25, 2010

MWANAFUNZI AFIA MAJINI

Mwanafunzi wa Darasa la sita katika Shule ya Msingi Manzese, jijini Dar es alaam, Ally Omary leo mchana aliopolewa na wasamaria baada ya kuzama kwenye bwawa la maji lenye kina kirefu lililopo karibu na viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilichopo Mlimani. Katika zoezi hilo Kikosi cha Uokoaji cha Zimamoto cha Halmashauri ya Jiji kilijaribu kuutafuta mwili wa mtoto huyo bila mafanikio mpaka walipotokea wasamaria wanaojua kuogelea na kuamua kupiga mbizi kuutafuta mwili huo.


Umati ukitafakari jinsi ya kuusaka mwili wa mwanafunzi huyo.
Kikosi cha uokoaji kikingia kazini.
Waokoaji wa kikosi cha Halimashauri ya Jiji wakitumia miti kuusaka mwili wa marehemu lakini waliambulia patupu na kunusurika kupigwa na wananchi wenye hasira.
Ulinzi uliimarishwa eneo la tukio kuwadhibiti wananchi wenye hasira waliotaka kutoa kipigo kwa waokoaji hao baada ya kuwaona huduma zao si lolote.
Wakati zoezi la utafutaji mwili likiendelea ulionekana mwili wa kukualiyechinjwa ukielea kwenye bwawa hilo.


Mwili ukiendelea kutafutwa.
Baada ya kuonekana huduma za waokoaji hao ni za ubabaishaji wasamaria hawa walijitosa kwenye bwawa hilo na kufanikiwa kuupoa mwili wa marehemu.
Mmoja kati ya wasamaria waliojitolea kuusaka mwili huo akiwa kazini.
Wasamaria wakiwa na mwili wa marehemu baada ya kuupoa Kikosi cha Halmashauri kilipochemka.
Mwili wa Marehemu.
Kikosi cha Halmashauri ya kikiondoka eneo la tukio.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake