
Wazee na wawakilishi wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo wamefunga njia ya magari kwa kulala Barabarani mbele ya Mahakama Kuu iliyoko mtaa wa Kivukoni na kuzuia magari kupita katika eneo hilo kwa kile walichodai kutosomwa kwa hukumu ya kuidai Serikali mafao yao baada ya jaji aliyekuwa akisikiliza kesi yao, Mh. Jaji Njegafibili Mwaikugile wa Mahakamu Kuu kujitoa katika siku ya hukumu. Hadi mtandao huu unaondoka eneo la tukio mchana huu, wazee hao walikuwa bado wamelala hapo wakidai mpaka kieleweke kama wanavyoonekana pichani!

...lango la kuingilia Mahakama Kuu likiwa limefungwa

...akina mama wakiwa wamelala
...akina baba nao wakiwa wamelala
PICHA: Issa Mnally/GPL

No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake