Tuesday, December 21, 2010

Akutwa amefia ndaniya Lifti Dar!

Mtu mmoja mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 40 hadi 45 ambaye jina lake halijatambulika amekutwa amekufa katika lifti ya jengo la Posta House lililopo jijini Dar es Salaam.

Mtu huyo ambaye alikutwa chini ya lifti ya jengo hilo amekufa zaidi ya siku tatu nyuma na maiti kuokolewa na kikosi cha zimamoto na uokoaji cha Kampuni ya Ultimate kwa kushirikiano na kikosi cha zimamoto wilaya ya Temeke.


Kabla ya kutolewa kwa maiti hiyo kikosi cha uokoaji na zimamoto cha Temeke kilishindwa kutoa maiti hiyo hadi gari la kampuni ya Ultimate lilipowasili na kuanza kutoa maiti hiyo.

Kabla ya zoezi hilo kuanza iliwalazimu waokoaji hao kuzama chini ya lifti hiyo huku wakiwa na vifaa mbalimbali na mitungi ya gesi ambapo waliikuta maiti hiyo ikiwa imeharibika vibaya hadi kufikia hatua ya kutoka ngozi yake yote na kubaki mweupe.

Kwa mujibu wa mmoja ya wafanyakazi wa jengo hilo ambaye alikataa kutajwa jina lake alisema, asubuhi walifika kazini na kuanza kusikia harufu kali ikitoka katika lifti ambapo walifikiria ni harufu ya panya.

Aidha, shuhuda huyo alisema kadri muda ulivyozidi kwenda harufu iliongezeka ndipo walipoamua kumwita fundi mkuu wa lifti wa jengo hilo ili afungue na kumtoa panya huyo ambaye alikuwa akisumbua kwa harufu kali hata hivyo baada ya fundi kufungua alikuta ni mtu.
                                                      
                                                     CHANZO:DARHOTWIRE

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake