Leon Bahati
HATIMAYE dunia sasa inaweza kuwa na matumaini ya kuondokana na ugonjwa hatari wa Ukimwi baada ya chanjo ambayo iligunduliwa mwezi Julai mwaka huu na wanasayansi wa Marekani, kuanza kufanyiwa majaribio.
HATIMAYE dunia sasa inaweza kuwa na matumaini ya kuondokana na ugonjwa hatari wa Ukimwi baada ya chanjo ambayo iligunduliwa mwezi Julai mwaka huu na wanasayansi wa Marekani, kuanza kufanyiwa majaribio.
Wagunduzi wa kinga hiyo walitamba mwezi Julai kuwa chanjo hiyo ina uwezo wa kukabiliana na Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa asilimia 90, na sasa wanahamasisha watu ambao hawajaambukizwa Ukimwi kujitokeza katika majaribio ya chanjo hiyo.
Hatua ya kufanyiwa majaribio kwa kinga hiyo imekuja baada ya wagunduzi hao ambao ni Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (Niaid) ya nchini Marekani kufanikiwa kuhamisha teknolojia ya dawa hiyo kutoka kwenye maabara.
Hatua ya kufanyiwa majaribio kwa kinga hiyo imekuja baada ya wagunduzi hao ambao ni Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Kuambukiza na Mzio (Niaid) ya nchini Marekani kufanikiwa kuhamisha teknolojia ya dawa hiyo kutoka kwenye maabara.
Kwa mujibu wa taarifa ya Niaid iliyotumwa kwa Mwananchi wiki iliyopita, majaribio ya chanjo hiyo yatawajumuisha maelfu ya watu duniani kote na wengi wanahamasishwa kujitokeza ili kufanikisha utekelezaji wa hatua hiyo.
Mkurugenzi wa Niaid, Profesa Anthony Fauci anaeleza kwenye taarifa hiyo kwamba anatarajia majaribio hayo yanaiingiza dunia katika zama mpya za kuvikabili virusi vya ukimwi.
Mkurugenzi huyo pia anawataka watu kujitokeza kwa wingi kujitolea kufanyiwa majaribio, kwa kuwa hatua hiyo itaifungulia njia taasisi yake kupata kibali cha Shirika la Afya Duniani (WHO) cha kuanza kutumika kwa dawa hiyo duniani kote.
"Mafanikio haya hayawezi kuja bila maelfu ya watu duniani kote kujitolea katika kuunga mkono majaribio yetu," anasema Profesa Fauci.
Ingawa majaribio haya yatafanyika dunia nzima, alisema washiriki lazima wasome kwa ufasaha na kuelewa maelezo juu ya majaribio yake.
Kinga hiyo inatokana na tangazo la Niaid walilolitoa mwaka huu kwamba wamefanikiwa kugundua chembechembe za kinga VRC01 na VRC02 katika mwili wa binadamu ambazo zina uwezo wa kukabiliana kikamilifu na aina zote za VVU.
Baada ya ugunduzi huo, wanasayansi hao walisema kazi yao kubwa ni kutengeneza aina ya chanjo ambayo mtu mwenye afya akipatiwa, mwili wake utatengeneza VRC01 au VRC02.
Taarifa ya Niaid pia inaeleza kwamba chanjo hiyo inaweza kuwasaidia watu ambao tayari wameathirika, lakini afya zao zikaimarika baada ya kutumia vizuri dawa za kupunguza makali ya VVU.
Atakayepatiwa chanjo hiyo, Profesa Fauci anasema, mwili wake utakuwa imejijengea chembechembe kinga za kudumu maishani mwake na hawezi kuathiriwa na VVU hata kama atajamiiana na muathirika.
Mbali na majaribio ya VRC01 na VRC02, Profesa Fauci alisema kuna aina nyingine sita za chembechembe kinga zilizogunduliwa na wanasayansi wengine duniani ambazo pia Niaid inasimamia majaribio yake.
Profesa Fauci alisema yapo majaribio ya dawa nyingine za kukabiliana na VVU ambayo Niad pia inayafanya lakini kipaumbele cha watakaojitolea kimetolewa kwa Wamarekani.
Dawa hizo alisema ni ya maji ambayo wanasayansi wamebaini kuwa ikitumika kikamilifu kwenye uke itazuia maambukizo ya VVU wakati wa tendo la ndoa.
Aina nyingine ni dawa kwa waathirika wa Ukimwi pamoja na Kifua Kikuu ambayo Profesa Fauci anaielezea kuwa inatarajiwa kutoa ahueni kubwa kwa wanaosumbuliwa na maradhi hayo.
Dawa hiyo haitofautiani na dawa nyingine za kupunguza makali ya VVU, lakini Profesa Fauci anaelezea tofauti yake kwamba inaweza kutumiwa na mgonjwa ambaye yuko katika hali mbaya kutokana na kinga kupungua na wakati huo huo akawa na kifua kikuu.
Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, kabla ya kugunduliwa kinga wagonjwa wa namna hiyo walikuwa na nafasi ndogo ya kuishi kwa sababu iliwapasa kwanza watumie dawa ya kifua kikuu kwa wiki nane kabla ya kuanza kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi.
Anauelezea muda huo wa wiki nane kuwa ulikuwa unatoa nafasi ndogo ya mgonjwa kuhimili kasi ya mashambulizi ya VVU wakati huo ambao kinga yake imeathirika vibaya.
Lakini Profesa Fauci anasema: "Dawa hii iliyogunduliwa na wanasayansi nchini Cambodia inaokoa maisha ya muathirika aliye katika hali mbaya".
Anafafanua kuwa "hii inatokana na dawa hiyo kuweza kutumika wiki mbili baada ya mgonjwa kuanza kutumia dawa za kifua kikuu badala ya kusubiri mpaka zipite wiki nane".
Profesa Fauci alisema muathirika yeyote anakuwa katika mazingira ya kuambukizwa kirahisi kifua kikuu kwa sababu mwili wake ni dhaifu katika kujikinga na maradhi.
Profesa Fauci ambaye pia ni mshauri mkuu wa afya Ikulu ya Marekani, anasema anajivunia uwezo wa taaisi yake katika kusimamia kikamilifu utafiti na sasa dunia inashuhudia mapinduzi makubwa katika mchakato wa kusaka tiba ya ugonjwa huo ambao ni tishio kwa uchumi wa dunia kutokana na kukosekana kwa tiba ya kuaminika.
Alisema tafiti hizo zimefanywa na wanasayansi kwa miaka 15 iliyopita na zimeonyesha kuwa mafanikio ya kukabili VVU ambavyo viligunduliwa miaka 1980.
CHANZO:MWANANCHI
No comments:
Post a Comment