Saturday, December 18, 2010

Gbagbo awafukuza wanajeshi wa UN

Rais anayetetea kiti chake nchini Ivory Coast Laurent Gbagbo amewataka wanajeshi wote wa nje kuondoka nchini humo mara moja, na hivyo kuzidisha hali tete iliyofuatia uchaguzi wa urais mwezi uliopita.
Gbagbo
Gbagbo na Ouattara
Msemaji wake amewatuhumu wanajeshi wa Umoja wa Mataifa na majeshi ya Ufaransa kwa kusaidiana na waasi wa zamani.

Umoja wa Mataifa na na nchi nyingine zimemtabua Alassane Ouattara, mabaye ni hasimu wa Bw Gbagbo, kuwa ndio mshindi wa uchaguzi wa urais katika kura zilizopigwa Novemba 28. Bw Gbagbo anasisitiza kuwa yeye ndio mshindi.
Jeshi
Mwanajeshi anayemuunga mkono Gbagbo katika mitaa ya Abidjan
Bw Ouattara hivi analindwa na Umoja wa Mataifa katika hoteli moja mjini Abidjan.
Umoja wa Mataifa, Marekani na mkoloni wa zamani wa Ivory Coast, Ufaransa, pamoja na Mungano wa Afrika wamemtaka Bw Gbagbo kuachia madaraka.
lakini Bw Gbagbo amesema wizi ulifanyika katika uchaguzi huo na waasi ambao bado wanadhibiti upande wa kaskazini tangu baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2002-03.
Wafuasi wa Bw Ouattara wametishia kungia mitaani kuandamana, kufuatia mapigano yaliyosababisha vifo vya watu 20 mjini Abidjan siku ya Jumanne.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake