ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, December 22, 2010

Tibaijuka avunja ukuta Palm Beach

Profesa Tibaijuka
Mwandishi Wetu
HATIMAYE Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka ametekeleza azma yake ya kuvunja ukuta uliojengwa kwenye kiwanja namba1006 kilichoko Upanga jirani na Hoteli ya Palm Beach,  jijini Dar es S alaam

Kazi ya kuvunja ukuta huo ilifanyika jana jioni kuanzia majira ya saa 1:00 usiku na ilidumu kwa takriban nusu saa tu.
Kazi ya kuvunja ukuta huo ilifanywa kwa matingatinga matatu na malori kadhaa chini ya usimamizi wa askari wa jiji na polisi.

Hata hivyo wakati ukuta huo unavunjwa mmiliki wake Taher Muccadam ambaye alitishia kumshtaki waziri Tibaijuka, alikuwa hayupo."Kazi hiyo haikuchukua muda kwani kulikuwa na vifaa vya kutosha na walikusanya kila kifusi na kukibeba," chanzo cha habari kutoka eneo la tukio kililieleza gazeti hili muda mfupi kabla halijaenda mtamboni

Kwa mujibu wa chanzo hicho cha habari, mbali na kuvunjwa ukuta huo, askari hao pia walivunja ukuta wa kiwanja kilichoko eneo la Gymkhana karibu na Hospitali ya Hindu Mandal.


                                       CHANZO:MWANANCHI

2 comments:

Anonymous said...

You did your job and I am proud of you. I hope you will keep on doing the right thing.

Anonymous said...

ndugu mhe hongera umeonesha mfano na kutokua na woga keep it up how i wish all other miniters would have to follow your step and be so serious in whatever choice they do.Meya Seattle wa