ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 30, 2010

Takriban watu 20 wafa maji Tanzania


Zaidi ya abiria 20 wanahofiwa kufa maji katika mkoa wa Mtwara kusini mwa Tanzania kutokana na ajali ya boti ambayo haijajulikana jina lake.
Boti hiyo ambayo inakadiriwa kuwa na watu 28 imezama leo mchana katika bahari ya Hindi.
Awali mwandishi wetu Josephat Mwanzi alizungumza na kamanda wa polisi wa Mtwara Steven Buyoya aliyekuwepo kwenye eneo la tukio akisema watu wanane wameokolewa lakini mmoja miongoni mwao amefariki dunia.
Boti, Tanzania
Boti, Tanzania
Wakati kazi ya uokoaji ikiendelea, mmiliki wa boti hiyo ambaye hajajulikana mpaka sasa amekimbia pamoja na kapteni wake.
Boti hiyo kutokana na kamanda Buyoya ina uwezo wa kubeba abiria 18 lakini pia hujikuta ikijaa kutokana na mizigo zikiwemo basikeli.
Boti hiyo inayomilikiwa na mtu binafsi aghlabu hubeba wavuvi na wachuuzi wadogo wadogo.
Shughuli ya kuokoa watu hao imesitishwa kutokana na kiza na itaendelea siku ya Jumamosi saa mbili asubuhi

Kuzuia ndoa ya wake wengi yazua tafrani


Mswada unaokusudia kupiga marufuku ndoa za wake wengi Malawi umeamsha hasira kali kutoka kwa jamii ya kiislamu nchini humo.
Msemaji wa jumuiya ya kiislamu ya Malawi, Imran Shareef Muhammed, ameiambia BBC mswada huo ukipitishwa utawabagua waislamu wachache waliopo nchini humo.
Jacob Zuma na wake zake
Jacob Zuma, Rais wa Afrika Kusini ana ndoa ya wake wengi
Bw Muhammed amesema kuna takriban asilimia sita zaidi ya wanawake kuliko wanaume Malawi.
Na iwapo ndoa za wake wengi zikipigwa marufuku, wanawake wengi watabaki bila kuolewa na hivyo kujiingiza katika ukahaba.
Siku ya Alhamisi, waziri wa jinsia wa Malawi alisema hatua ya kupiga marufuku ndoa hizo ni muhimu ili kuzuia wanawake kunyanyaswa katika ndoa za wake wengi.

10 wafa katika maporomoko Kenya


Watu kumi wamethibitishwa kufa na wengine 15 hawajulikani walipo kufuatia maporomoko ya udongo katika wilaya ya Marakwet, magharibi mwa Kenya.
Maporomoko
Maporomoko ya udongo Brazil. Hali kama hiyo imetokea Kenya.
Maporomoko hayo yametokea alfajiri ya Ijumaa. Idadi kubwa ya waliokufa ni watoto. Wakazi wa huko wanasema maporomoko hayo yametokea baada ya mvua kubwa kunyesha.
Miili ya watoto wenye umri wa miaka 10 hadi mitatu iliyosombwa na maji imepatikana kwenye mto katika eneo hilo.
Shughuli za uokoaji zinafanyika katika eneo hilo lenye milima.
watu saba wamejeruhiwa katika tukio hilo na wamepelekwa hospitali.
Shirika la misaada la Red Cross na kitengo cha kukabiliana na majanga cha serikali ndio wanaongoza shughuli hiyo.
Marakwet ipo katika eneo karibu na bonde la ufa, na wakazi wa eneo la tukio wanaishi karibu na mto.

Mjue Mwasiti Almasi



Wiki iliyopita tulimshuhudia Mwanamuziki wa Miondoko ya Dansi Bongo, Waziri Sonyo akiambaa na mistari pande hizi. Leo ndani ya uwanja huu tutakula kitu laivu bila chenga kutoka kwa staa wa muziki wa Kizazi Kipya aliye zao la Jumba la Kukuza Vipaji (THT) ambaye kwa sasa ni Balozi wa mpango mzima wa vita dhidi ya Malaria Bongo. Huyu si mwingine bali ni Mwasiti Almasi.
Kabla ya kulisongesha jahazi mbele zaidi, Mwasiti alizaliwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, jijini Dar. Kuhusu ‘eji’ yake, sistaduu Mwasiti aligoma katakata kusema hadi hapo atakaporejea mwana wa Adamu kuchukua walio hai na wafu.

Wazazi wake ni wenyeji wa Kigoma Ujiji. Mwasiti aligonga Shule ya Msingi Mwenge, jijini Dar na baadaye Mbezi High School kwa masomo ya sekondari.
Nisikumalizie uhondo, kwa mengi zaidi tusonge pamoja;

TQ: Niaje Mwasiti? Ndoto ya kuwa mwanamuziki uliipata ukiwa wapi na THT ulijiunga mwaka gani?
Mwasiti: Niko poa sana mtu wangu. Kusema kweli tangu nikiwa shule ya msingi na baadaye sekondari, nilikuwa napenda sana muziki, ‘so’ naweza kusema nilikuwa na ndoto ya kuwa mwanamuziki tangu utotoni.

Ili kukamilisha ndoto zangu nilijiunga THT tangu mwaka 2006 nikiwa na lengo la kukuza kipaji changu cha muziki huku nikisubiria kuendeleza libeneke la masomo.

TQ: Ni nani waliokuvutia nje na ndani ya nchi kuingia kwenye muziki?
Mwasiti: Kwa nje nilikuwa navutiwa sana na kazi za Celine Dion. Kwa hapa Bongo ni Judith Wambura Mbibo ‘Binti Machozi’. Kusema kweli huwa napenda sana kazi zao.

TQ: Ndani ya ‘gemu’, malengo yako hasa ni nini? Na nyimbo zako huwa unatunga mwenyewe au unatungiwa?
Mwasiti: Tukizungumzia suala la malengo, nahitaji kuwa msanii wa kimataifa na nyimbo zangu zote natunga mwenyewe na wala sitegemei kutungiwa kwa kuwa najiamini na nina kipaji. Mimi silazimishi kama wanavyofanya wengine.

TQ: (akivuta pumzi) Je, umeolewa? Na kama hujaolewa huna mpitanjia ambaye unabadilishana naye mawazo?
Mwasiti: Duh! umeanza maswali nisiyoyapenda. ‘Inshort’ sijaolewa wala sina mchumba, hata huyo mpitanjia unayemsema sina. Mpango huo kwa sasa siufikirii. Siku nikiwa tayari nitautangazia umma.

TQ: Baadhi ya wasanii hawapendi kuishi mikoani walikozaliwa na wengine wanathubutu kukataa kutaja sehemu wanazotokea. Je, kwa upande wako hilo limekaaje?

Mwasiti: Katika maisha yangu sijawahi kuchagua pa kuishi, isitoshe mimi ni kioo cha jamii hivyo sehemu yoyote ile ambayo naamini inaendana na mazingira ya kazi yangu, iwe mjini au kijijini.

TQ: Je, unaishi kwako, nyumbani kwenu au umepanga?
Mwasiti: Haa jamani! Mbona maswali ya kichokozi sana? Haya bwana, naishi kwangu maeneo ya Mwenge, sijapanga, naishi kwenye nyumba ya familia.

TQ: Nikirudi nyuma, nakumbuka ulisema huna mchumba wala hutegemei, je, unataka kuniambia huwa hawakutokei?

Mwasiti: Dah wewe naye! Hivi kweli kuna mwanamke asiyetongozwa? Mimi najua kila mwanamke mzuri lazima atongozwe hata kama ni mke wa mtu kinachotakiwa ni namna yeye anavyojiweka tu. Natongozwa sana lakini niko ‘smart’ ile mbaya.

TQ: Mara nyingi mwanamke kuwa na bifu na mwenzake ni suala la kawaida, je, kwa upande wako uliwahi kuwa na bifu na msanii mwenzako au mtu mwingine yeyote?

Mwasiti: Niliwahi kukorofishwa na rafiki yangu wa kike nikiwa shuleni. Kusema kweli hadi leo bado nina kinyongo naye ingawa siku zimepita.
TQ: Je, siku ukibahatika kuwa na familia ungependa kuwa na idadi ya watoto wangapi na wa jinsia gani?

Mwasiti: Ikitokea hivyo, mara nyingi kutokana na hali ya kiuchumi. Napenda kuwa na familia ya watoto wawili tu. Wa kiume na kike. Hapo ndipo nitakuwa nimetimiza furaha yangu.
TQ: Watoto hao ungependa wawe wa baba mmoja au tofauti, na wawe wanamuziki kama mama yao au watakavyopenda?

Mwasiti: Siku zote napenda watoto wangu wawe wa baba mmoja mstaarabu anayependa watoto, kuhusu fani yangu, hilo sitawaingilia ila nikiona anapenda kuwa mwanamuziki, basi nitamsapoti

Thursday, April 29, 2010

Makamu Rais wa Uganda matatani


Uchunguzi uliofanywa na bunge la Uganda kuhusu matumizi mabaya ya fedha za serikali umependekeza kuwa Makamu wa Rais, Gilbert Bukenya, na mawaziri kadhaa na mawaziri kadhaa wanatakiwa kufunguliwa mashtaka.
Madai dhidi yao yanatokana na zabuni za serikali zilizotolewa kwa ajili ya mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Madola uliofanyika Uganda mwaka 2007.
Gilbert Bukenya, makamu wa rais wa Uganda.
Gilbert Bukenya, makamu wa Rais wa Uganda anakabiliwa na tuhuma nzito za ubadhirifu.
Uchunguzi uliofanywa na bunge la Uganda kuhusu matumizi mabaya ya fedha za serikali umependekeza kuwa Makamu wa Rais, Gilbert Bukenya, na mawaziri kadhaa wanatakiwa kufunguliwa mashtaka.

Kamati ya bunge ya mahesabu ya umma imedai kuwa Bw Bukenya alikiuka taratibu katika kuagiza magari maalum ya kutumiwa na viongozi wakati wa mkutano huo. Siku ya Alhamisi, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, aliitwa mbele ya bunge kujitetea. Haijajulikana aliongea nini, lakini lengo lilikuwa kubaini endapo naye alihusika na kashfa hiyo.
Ripoti ya awali ya kamati hiyo ya bunge inasema, Makamu wa Rais Gilbert Bukenya ambaye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya mawiziri iliyokuwa inapanga mkutano huo alikiuka sheria za kutoa zabuni na lazima awajibike.

Tuhuma nzito

Kamati hiyo ya bunge iliyoidhinishwa na Rais Museveni inasema kulikuwepo na udanganyifu katika utoaji wa zabuni kwa watu binafsi na makampuni yaliyotoa huduma wakati wa mkutano huo wa Jumuiya ya Madola uliosababisha serikali kupoteza mamilioni ya dola.
Wana kamati wanasema hatua ya Makamu wa Rais Bukenya ya kukiuka sheria inabainisha jinsi serikali ilivyoonyesha ujeuri na wamesikitika kuwa alikataa kufika mbele yao kujitetea dhidi ya tuhuma hizo.
Mawaziri wengine waliojikuta matatani baada ya uchunguzi huo ni yule wa mambo ya nje, wa utalii vile vile barabara na ujenzi

Viongozi wajinadi mdahalo wa mwisho Uingereza


Viongozi wa vyama vikuu vya kisiasa nchini Uingereza wakiwa katika mdahalo wa mwisho.
Ilikuwa ni fura ya mwisho kwa Cameron, Clegg na Brown kujinadi kabla ya uchaguzi wiki moja ijayo.
Katika mdahalo wa mwisho kuwapambanisha viongozi wa vyama vikuu vya kisiasa nchini Uingereza uliofanyika Alhamis usiku, Waziri mkuu wa sasa, Gordon Brown, alitumia fursa hiyo kuwaomba wapiga kura wasifanye makosa kubadilisha serikali inayoongozwa na chama cha Labour.
Kiongozi huyo wa chama cha Labour, ambaye chama chake kipo nafasi ya tatu kwa mujibu wa kura za maoni, alionya uwezekano wa chama cha Conservative kuunda serikali ya mseto na chama cha Liberal Democrat, akisema kwa kufanya hivyo mipango ya kufufua uchumi wa nchi itaathirika.
David Cameron alimlaumu Bw Brown kwa kujaribu "kuwatisha" wapiga kura akaeleza kuwa chama chake cha Conservative kitaleta mabadiliko yanayohitajika.
Nick Clegg aliwasihi wapiga kura "kuchagua mustakabal wanaoutaka kwa uhakika"

Nyama Choma Crystal Club Jumapili May 2/2010



MASIPESHALISTI WA BBQ WAMEAGIZWA MAALUMU KWA SIKU HIYO YA JUMAPILI KAZI KWENU 


LATIFA ANAWAALIKA WOTE KWENYE 


NYAMA CHOMA YA BESIDEI YAKE 


JUMAPILI SAA 10:30 JIONI(4:30PM) 


CRYSTAL NIGHT CLUB NA BAADAE NI DJ 


KAY NA DJ VIQ KWENYE REGGAE SUPER 


SUNDAY MPAKA LIAMBA TAFADHALI 


ZINGATIA MUDA,ASANTE NA KARIBUNI 


WOTE

Ukisikia market la Tandale ndo hili sasa,waaweza kuta wachuuzi kama jiti (100) na wote wanauza bidhaa aina moja

Penzi lenu halina amani kisa, simu zenu za mkononi?


Ni wiki nyingine tunakutana tena kupitia safu hii ambayo kimsingi tunakumbushana na kuelimishana juu ya mambo mbalimbali yanayogusa maisha yetu ya kimapenzi. Naamini wewe msomaji wangu umzima bukheri wa afya na uko tayari kabisa kupitishia macho kile ambacho nimekuandalia kwa siku hii ya leo.
Mara kwa mara nimekuwa nikiandika makala zinazohusu
tatizo la simu za mkononi kwa wapenzi kwani limekuwa ni kama wimbo wa taifa sasa.

Tumekuwa tukishuhudia wapenzi wakiachana, walio katika ndoa wakitengana na wengine kukorofishana kila mara huku baadhi wakibaki katika uhusiano wa mashaka, chanzo kikiwa ni simu za mkononi.
Aidha, nimekuwa nikipokea simu nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali wakielezea namna ambavyo chombo hiki cha mawasiliano kimekuwa kikisababisha mtafaruku kati yao na wapenzi wao.

“Sina amani kaka yangu, mimi na mpenzi wangu tumekuwa ni watu wa kugombana kila wakati kwa sababu ya simu yangu ya mkononi, mara nyingi anahisi namsaliti na kila ninapoongea na simu anadhani naongea na wanaume zangu, naumia sana hadi wakati mwingine kuona bora nisiwe na simu kwani inaweza kusababisha nikaachana na mpenzi wangu wakati bado nampenda,”anaeleza Maria wa Dodoma.
Kwa kweli simu za mkononi kwasasa zimekuwa ni sumu katika uhusiano na hii inatokana na baadhi ya watu wasiowaaminifu kuzitumia katika kuwasaliti wapenzi wao.

Nilichodhamiria kukiandika wiki hii ni jinsi unavyoweza kumfanya mpenzi wako asihisi kwamba unamsaliti kwa kutumia simu yako ya mkononi. Nikuhakikishie tu kwamba, kwa kuzingatia haya nitakayoandika na kama mpenzi wako ni mtu mwenye uelewa mkubwa, simu zenu za mkononi haziwezi kuwaletea matatizo.
Kwanza, kama kweli wewe ni muaminifu kwa mpenzi wako unatakiwa kujiamini kila unapokuwa karibu naye na wala usioneshe kujishtukia. Wapo ambao kila wanapokuwa na wapenzi wao, wakipata sms tu, watajificha ili wasome haraka kisha wafute. Wakipigiwa wakiwa na wapenzi wao kama hamjui anayempigia basi atakata na kuizima kabisa.

Hivi unapofanya hivyo unataka mpenzi wako akufikirieje? Utamjengea mazingira gani ili akuamini na kutohisi kuwa kuna mshikaji mwingine anakuzingua ama una uhusiano naye wa kimapenzi kwa siri?
Kimsingi kujishtukia kwako pale unapokuwa na mpenzi wako kunaweza kukuharibia. Ndiyo maana nasema, kama kweli unampenda huyo uliyenaye usiweke mazingira ya usiri kwenye simu yako. Wakati mwingine kuwa tayari kumjibu pale atakapokuuliza ni nani aliyekupigia simu au ujumbe huo unatoka kwa nani. Siyo kila mara atakuuliza lakini pale atakapokuuliza mjibu.

Pili, unatakiwa kutambua kuwa wewe ni mpenzi/ mke au mume wa mtu. Hivyo basi siyo busara kujirahisi na kumpa kila mtu tena wa jinsia nyingine namba yako ya mkononi. Itoe kwa watu muhimu ambao hata siku wakija kukupigia simu ukiwa na mpenzi wako iwe rahisi kujieleza.
Unaweza kumkuta msichana anakutana na mvulana na anatongozwa, awali anakataa lakini mwisho anaombwa namba yake ya simu na anaitoa. Utamuelewa vipi msichana kama huyu? Huyu ndiye wale nataka sitaki kama hujui.

Hivi wewe huelewi kwamba wanaume wengi siku hizi wakishapata namba ya simu tu wameshamaliza kazi? Nasema wameshamaliza kazi kwa sababu ni wataalam wa kutongoza kupitia kwenye simu.
Sasa siku mtu kama huyo akikutumia ujumbe wa kimapenzi na mpenzi wako akauona utamwelezaje? Hawezi kukuelewa.
Tatu,unatakiwa kuwa makini sana na watu wanaokutaka kimapenzi. Hawa hata usipowapa namba yako ya simu wanaweza kufanya juhudi za kuipata kupitia kwa watu wako wa karibu. Kwa maana hiyo basi, wanaokusumbua ni vyema ukamweleza mpenzi wako.

Hiyo itakusaidia! Lakini kama jamaa anakuimbisha kila unapokutana naye kisha unanyamaza, siku mpenzi wako atakapokuja kuwakuta sijui utamueleza nini akuelewe! Itakuwa ngumu.
Hata wewe mwanaume kama kuna mwanamke anakushobokea, mpe taarifa laazizi wako kwamba unajua demu fulani ananisumbua. Kimsingi usimfiche mpenzi wako katika kila jambo kwani waswahili wanasema, mficha maradhi kifo kitakuja kumuumbua!
Kwa leo inatosha. Kwa ushauri wowote wa maisha ya kimapenzi usisite kuwasiliana nami kupitia simu namba 0653548420 au barua pepe:zekaima@yahoo.com

ADHA YA MASIKA, DAR HAIKALIKI


Jangwani
Mvua za masika zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam leo zimesababisha baadhi ya wakazi wake kukimbia makazi yao kufuatia mafuriko makubwa yaliyozikumba nyumba zao.
Mchana huu wanahabari wetu walitembelea maeneo mbalimbali ya ya jiji na kujionea ‘live’ baadhi ya nyumba zikiwa haziingiliki kufuatia kuzingirwa na maji. Sehemu zilizotembelewa kuona madhara ya mvua hizo ni:
Jangwani

Bonde la Muhimbili

Kinondoni Mkwajuni

Nyumba ya mganga maarufu jijini, Dk. Midinye, iliyopo Jangwani, nayo ni moja zile zilizokumbwa na adha hiyo.

PICHA: RICHARD BUKOS NA KYALAA SEHEYE

Truly Strange Stage Wear


The Ferginator

Space Bride Beyonce

Keri Hilson's Graphic Onesie

Rihana's Half-Reveal

Janet Jackson's Tronsuit

Lady Gaga's Geometric Panty Suit

Beyonce's Queen Glitter B

Katy Karousel
Image
Gari dogo lenye namba za usajili T 779 ASH likiwa limegonga kwa nyuma daladala lenye namba T 916 ABN katika barabnara ya Azikiwe Dar es Salaam wakati gari hilo dogo likitokea mtaa wa Garden jana mchana. (Picha na Mroki Mroki)

Stars Yapata Mfadhili

Mr.Mwasalwiba mwenye kampuni ya MT.ZION.INC ambayo ndio itakua mzamini wa Stars United,Mr Mwasalwiba ameahidi uzi mpya kwa Timu hiyo,Mr Mwasalwiba akishirikiana na Vanessia Kitwara bila kumsahau John Sitta walifanya mauaji ya Birthday party ambayo ilivunja rekodi kwanza kwa kua party ya kwanza kualika watu bila kadi,
pili,party hii ilivunja rekodi yakua na vinywaji vingi na vyakula kuliko kawaida ya party zilizowahi kufanyika na zitakazokuja kufanyika,wataalamu wa mambo wanasema hii haijawahi na haitawahi kutokea labda wao wenyewe waamue kuvunja rekodi yao.
tatu,kufanya party kama ile kwa kualika watu kwa text message,bila kujali ni Mbongo Mkenya,Mpopo n.k..
nne,siku zote party kama hizi watu hufunga menyu kwenda nazo nyumbani lakini hii ilikua tofauti watu walifunga kanywaji tena tani yako.
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Viongozi,Daktari na Wachezaji kwa ujumla wanashukuru sana kwa wewe kujitolea kua Mfadhili wao,si rahisi kupata neno  la kushukuru litakalo lingana na wewe kukubali kuwa mfadhili wa timu,kusema Asante inaonekana haitalingana na huu uamuzi wako mkubwa ambao kamwe hautasahaulika,kwa wachezaji.Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa moyo wako wa kujitolea,
Kwa niaba ya wachezaji ni 
Mimi Mratibu Mully Chomba

Museveni kujieleza mbele ya tume


Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekubali kufika mbele ya tume ya uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za maandalizi ya mkutano wa Jumuiya ya Madola.
Taarifa kutoka ikulu ya rais imethibitisha Rais Museveni kupangiwa kukutana na tume hiyo wakati wowote.
Uganda iliandaa mkutano wa wakuu wa mataifa ya Jumuiya ya Madola (CHOGM) mwaka 2007 na kuhudhuuriwa kama kawaida na Malkia Elizabeth wa pili ambaye ni mkuu wa jumuiya hiyo.
Museveni
Rais Museveni ameapa kuadhibu yeyote atakayepatikana na hatia
'Rais aliruhusu'
Tume hiyo inachunguza madai kwamba fedha nyingi zilitumika vibaya kuandaa mkutano huo, ambapo rais Museveni anadaiwa kukubali matumizi zaidi kuliko fedha zilizotengwa kwa ajili ya mandalizi hayo.
Madai mengine katika sakata hilo ni matumizi ya dola milioni tano kununua vyombo vya mawasiliano, badala ya dola milioni tatu zilizoidhinishwa awali. Watu waliohojiwa na tume hiyo wamedai kuwa rais aliruhusu hatua hiyo.
Ununuzi wa magari
Aidha rais Museveni anatazamiwa kutolea maelezo madai ya fedha nyingi kutumika katika mahoteli na ununuzi wa magari.
Katika hotuba yake kwa taifa kwenye mkesha wa mwaka mpya, rais Museveni, ambaye ndiye ametaka kuwepo kwa tume hiyo, aliapa kuadhibu afisa yeyote wa serikali ambae atapatikana na hatia ya kutumia vibaya pesa za CHOGM.
Tume hiyo inakamilisha kazi yake, na kabla ya kufanya hivyo pia ilitaka kukutana na rais

Maafisa wakiri mashitaka Rwanda


Maafisa wawili nchini Rwanda wanaodaiwa kuunda kundi la kigaidi kwa lengo la kuhujumu nchi wamekiri mashitaka dhidi yao.
Maafisa hao Luteni Kanali Tharcisse Mbiturende na Luteni Kanali Habiyakare Noel wamekiri mashitaka hayo ambayo ni pamoja na madai ya kushirikiana na mwanasiasa Ingabire Victoire.
Ingabire Victoire ametangaza kuwania kiti cha urais katika uchaguzi utakaofanyika baadaye mwaka huu nchini Rwanda.
Ingabire
Ingabire Victoire amehusishwa na kundi la FDLR
Upande wa mashitaka umedai maafisa hao walikuwa wanatumukia jeshi la Rwanda kabla ya kujiunga na kundi la FDLR kwa lengo la kuvuruga usalama.
Ingabire Voctoire ambaye ni mkosoaji wa serikali alikuwa akitajwa sana, mapema wakati kesi ikianza.
Uhusiano wa karibu
Mwendesha mashitaka ameonesha ushahidi wa barua pepe, unaodhihirisha uhusiano kati ya maafisa hao wa kijeshi na Bi Ingabire. Aidha ushahidi wa mikutano iliyofanyika mjini Kinshasa na fedha walizotumiana umewasilishwa katika mahakama ya Gasabo, mjini Kigali.
Wakikiri mashitaka hayo, washukiwa hao wamekiri kuwa na uhusiano wa karibu na bi Ingabire na kusema aliwataka waunde kundi jipya, lakini walikamatwa kabla ya kutekeleza hilo.
Upande wa utetezi umetaka kujua kwa nini washukiwa hao walikamatwa mwezi Septemba mwaka jana, lakini wamefikishwa mahakamani miezi saba baadaye. Mwendesha mashitaka amesema utaratibu wa kisheria umefuatwa.

Wednesday, April 28, 2010

NABSHOW2010 IN VEGAS


MPWA HAYA NDIYO MAMBO YALIYOKUWEPO HUKO KWENYE RADIO AND TV SHOW (NABSHOW2010) HAPO LAS-VEGAS HAPO MKURUGENZI MSAIDIZI WA MAMBO JAMBO FM - ARUSHA BWANA SAID NASSOR AKIWA KATIKA HEKA HEKA ZA KUANGALIA MITAMBO MIPYA YA RADIO NA TV AMBAYO WANATAKA KWENDA KUFUNGA HIVI KARIBUN

U-KODAK MOMENT


Beach Boy akifurahia kupata kumbu kumbu wakati Stars ikiwa Mjini Cambridge,kulia ni Kheri Yahaya

Salaam kutoka Harvard University


KUTOKA SHOTO KABAMBII" MOSES (NY,NY),DIDI VAVA,HARVARD UNIVERSITY STUDENTS ;DR. SHAO, DR. MWIRU & DR. MATECHI

wachezaji Stars united wakiwa mapunziko Cambridge,MA,kutoka kushoto Ebra Nyagaly(NY),Denis Geofrey(NC),Abdul-Tif Maalim(NJ)

Simba kuanza na Atraco katika Kagame


Mabingwa wa soka wa Tanzania Bara, Simba SC
Na Mwandishi Wetu
MABINGWA wa soka wa Tanzania Bara, Simba wataanza harakati zao za kuwania Kombe la Kagame kwa kucheza na mabingwa watetezi Atraco ya Rwanda. Mei 17 mwaka huu mjini Kigali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatatu wiki hii na kusainiwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Nicholas Musonye, michuano hiyo itafunguliwa Mei 15 mwaka huu kwa mchezo utakaowakutanisha mabingwa wa Rwanda APR na Vital’O ya Burundi.

Mara baada ya mchezo wake dhidi ya Afraco, Simba itacheza mechi ya pili na Sofapaka Mei 20 mwaka huu kabla ya kumaliza hatua ya makundi kwa kupambana na timu ya Mamlaka ya Mapato Uganda siku tatu baadaye.
“Tumezialika timu za Heartland ya Nigeria na TP Mazembe ya DR Congo katika michuano hii. Tumezileta timu hizi ili kuongeza chachu ya ushindani,” alisema Musonye.

Michuano hiyo itagharimu kiasi cha dola 60,000 za Marekani ambapo ndani yake bingwa atapata dola 30,000, mshindi wa pili 20,000 na mshindi wa tatu atapata dola 10,000. Timu mbili zitakazoshika nafasi za juu katika makundi yote matatu na timu bora kutoka makundi hayo, zitacheza hatua ya robo fainali. Kundi A lina timu za ARP (Rwanda), TP Mazembe (DR Congo), Vital’O (Burundi) na TeIkom ya Djibouti, timu za kundi B ni Rayon (Rwanda), St. George (Ethiopia), Heartland FC (Nigeria) na Mafunzo ya Zanzibar, Atraco ya Rwanda, Simba (Tanzania), URA (Uganda) na Sofapaka ya Kenya zipo kundi D.

Usikilize moyo wako, lakini angalia usikudangaye!-2


Kama si Mungu, tusingekutana tena leo katika kona yetu ya kuelekezana mambo haya na yale juu ya kufanya maisha yetu kwa upande wa uhusiano yawe mazuri yenye kuvutia. Hatuna budi kumshukuru yeye, maana imempendeza kabisa sisi kukutana leo na kupeana elimu hii muhimu. Karibuni sana marafiki!
Leo nahitimisha mada iliyoanza wiki iliyopita, kama inavyosomeka hapo juu. Nilianza na kisa cha msomaji wetu, ambaye alieleza jinsi anavyosumbuliwa na mwanaume ‘kicheche’ambaye hajatulia kabisa. Wiki jana niliandika vipengele vitatu, kwa faida ya ambao hatukuwa nao ni pamoja na kuangalia kama mwenzi huyo anaweza kubadilika, umri wake kama unalingana na makosa yake na kama ni mwenzi sahihi.
Sasa tunaendelea pale tulipoishia...

NANI KAKWAMBIA UNA NUKSI?
Moyo unatudanganya sana rafiki zangu, lakini kumekuwa na mawazo mengine ya kitumwa yanayotawala hisia zetu bila kujua. Eti mtu anafikiria kwamba, kukaa bila kuolewa ni nuksi! Unajua kinachotokea? Anakubali kuwa na mwanaume yeyote hata kama ana matatizo, ili awe ameondoa nuksi.
“Rafiki zangu wote niliomaliza nao shule wameshaolewa, wadogo zangu nao wameolewa, nimebaki mimi tu, siwezi kumuacha huyu mwanaume hata kama ana matatizo. Nitaendelea kuvumilia ili niondoe hii nuksi,” haya ni baadhi ya mawazo ‘mgando’ yaliyomo katika vichwa vya wanawake wengi.
Jipe moyo dada yangu, huna nuksi. Tulia, pima mambo, kisha panga maisha yako ya baadaye, kama wewe huku ukimwachia Mungu kazi ya kukutafutia mume sahihi. Unadhani kwa nguvu zako utaweza?

UNADHANI HUVUTII?
Hili ni tope lingine lililopo vichwani mwa wanawake wengi, hawajiamini. Wanadhani wao si wazuri au hawavutii, kwahiyo wanapokuwa na mwanaume, wanahisi kama wamebahatika tu, hivyo hawataki kuachia bahati hiyo! Huko ni kujidaganya.
Wapo wanaoshinda kwenye vioo wakijitazama na kuhakikisha kama kweli ni wazuri, kwa bahati mbaya vioo huwapa majibu tofauti kidogo...kwamba si wazuri kiiivyo! Halafu kuna hizi filamu na video za wasanii wa Kizazi Kipya, basi kutwa nzima mwanamke anashinda akijifananisha na msanii fulani kwenye sinema.

Akiona aina ya wanawake wanaosalitiwa kwenye ndoa za kwenye hadithi za sinema au nyimbo za wasanii husika, hujifananisha nao! Si kweli. Wewe ni mwanamke mzuri, ambaye unapendeza kwa mwanaume wako atakayekupenda. Si rahisi kupendwa na kila mtu. Unaweza kuambiwa na mpenzi wako anakupenda, lakini mtu mwingine akashangaa, kwanini mwenzi wako anakupenda!
Kila mtu ana mzuri wake jamani. Hata hivyo, ili uwe mzuri ni lazima kwanza uanze kwa kujikubali wewe mwenyewe. Kwamba wewe ni bora, unavutia na umeumbwa kipekee. Unajua ukianza kuwaza hivyo, hata tembea yako itakuwa ya kike na kujiamini, utavaa vizuri na kujipamba sawasawa. Utavutia zaidi ya unavyofikiria.
Kubwa zaidi, hata afya yako itakuwa njema, maana mawazo yako si ‘mtindi’ tena!

KUOLEWA SI KILA KITU!
Kitu kibaya kingine kinachofikiriwa na baadhi ya wanawake ni kwamba kuolewa ni kila kitu! Mwanamke akishaolewa anakuwa amemaliza kila kitu. Hili si wazo baya sana, maana heshima ya mwanamke ni kuolewa. Lakini vipi kama utaolewa na mwanaume ambaye si sahihi, akutese, akutukane, akupige, akusimange na kukufanyia kila aina ya vitu vibaya? Si utakuwa mwanzo wa kuharibu maisha yako?
Heshima ya ndoa ni kuishi kwa amani na furaha, hapo utakuwa umekamilisha kipengele hicho sawia. Kama kijisehemu hicho hapo juu kinavyosema, ni bora kuandaa maisha yako mwenyewe, uwe na uhakika na kesho yako, ukiweka malengo na kuyatimiza taratibu, ili uwe mwanamke bora. Kuwa mwanamke bora ni mwanzo wa kuelekea kuwa MKE BORA.

UMIA MARA MOJA UFURAHI MILELE
Inawezekana kichwani mwako kuna mambo mengi, likiwemo la mapenzi ya dhati kwa mwanaume wako, lakini tayari amepoteza sifa za kuwa mume sahihi, uendelee kuwa naye? Hata kama unampenda sana, moyo unakusisitizia hivyo, lakini tayari taa nyekundu inawaka mbele yako.
Fanya maamuzi, bora uumie mara moja halafu ufurahi milele, maana kukubali machozi ya mara moja na kuachana na mtu ambaye ni kikwazo kwako, kutafungua mlango wa aliye bora kuingia. Utaonekana vipi kama hutoki nje? Tafakari!

ANZA UPYA
Tua mzigo, halafu anza kwa upya. Yupo mwanamuziki mmoja amewahi kuimba; Kuanza upya si ujinga! Ni kweli kabisa, hakuna uwendawazimu wowote katika kuanza upya hasa unapogundua kwamba kuna makosa uliyoyafanya. Inamaanika kwamba anayekubali kukosea na kutaka kuanza upya, huwa bora zaidi katika hicho anachorudia, maana tayari anakuwa ameshajua kosa lake lilikuwa wapi!

UPO HAPO?
Naamini umesoma vipengele vyote kwa makini, umeelewa na una kitu cha kufanya. Ni bora kama utakuwa upo upande wangu, ingawa pia si lazima, kulingana na uamuzi wako binafsi.
Ikiwa upo upande wangu, nina hakika utakuwa umefungua ukurasa mpya wa maisha yako ya uhusiano ukiwa na furaha na nguvu mpya. Usikubali kuteswa na mapenzi!
Mada imeisha.

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi ambaye anaandikia magazeti ya Global Publishers, unaweza kuwasiliana naye kwa simu 0712 170745 au waraka pepe HYPERLINK “mailto:joeshaluwa@yahoo.com” joeshaluwa@yahoo.com kwa maoni na ushauri zaidi.

Mvua zinazoendelea kunyesha Dar

Image
Magari yakipita katika dimbwi la maji lililopo katika barabara ya Nyerere karibu na Kiwanda cha Uchapaji cha Taifa (KIUTA) Dar es Salaam kufuatia mvua iliyonyesha jana. (Picha na Mroki Mroki)

Mapacha walioungana waeneza Uislam


Mapacha waliokuwa wameungana Cameroon
Mapacha waliokuwa wameungana wameleta baraka kwenye jamii yao.
Mapacha walioungana kutoka Cameroon Pheinbom na Shevoboh walionekana kama nuksi walipozaliwa, lakini mafanikio yao ya kutenganishwa na madaktari wa Saudi Arabia yamebadili kabisa maisha yao – na imani ya baadhi ya watu katika kijiji chao.
Walipozaliwa walikuwa wameungana kwenye kifua, tumbo na nyonga na baadhi ya wauguzi katika kijiji cha Babanki Tungo kilichopo kaskazini-magharibi mwa Cameroon, walishtushwa sana na hivyo kukimbia siku walipozaliwa.Kwa Maelezo Zaidi BOFYA HAPA

Kenya yapinga ripoti ya ajali ya ndege


Waokoaji wakiwa eneo la ajali ya Kenya Airways nchini Cameroon.
Ndege hiyo aina ya Boeing 737 ilikuwa safarini kutoka Cameroon kwenda Kenya.
Mzozo umeibuka kati ya Kenya na Cameroon kuhusu ripoti ya uchunguzi wa chanzo cha ajali ya ndege ya Kenya Airways iliyoanguka mwaka 2007.
Tarehe 5 mwezi Mei mwaka 2007, ndege ya Kenya Airways, ilianguka mara tu baada ya kuondoka katika uwanja wa Douala, Cameroon na kusababisha vifo vya watu wote 114 waliokuwemo ndani.

Ripoti hiyo inasema makosa ya rubani wa ndege hiyo huenda ndiyo yaliyosababisha ajali hiyo. Lakini serikali ya Kenya kupitia Naibu waziri wa uchukuzi, Amos Kimunya, inasema haikubaliani na ripoti hiyo.
Ripoti inaeleza kuwa naibu rubani alikuwa kijana mwenye umri wa miaka 23 na kwamba huenda kulikuwa na mgongano na kutoelewana kati ya kijana huyo na rubani mkuu aliyekuwa na umri wa miaka 52.
Serikali ya Kenya pamoja na wakuu wa shirika la ndege la Kenya Airways waliandaa kikao na wanahabari na kusema hawakubaliani na baadhi ya madai yaliyomo kwenye ripoti hiyo.

Kenya yataka mapatano na Dubai


Waziri wa mambo ya nje wa Kenya, Moses Wetangula yuko Dubai kujaribu kutuliza mvutano baada ya ndugu wa familia ya kifalme ya Imarati kurejeshwa nyumbani kwa kushukiwa kuwa magaidi.
Watu hao wanne walikuwa mapumzikoni katika pwani ya Mombasa wakati wa Pasaka, wakati maafisa wa uhamiaji walipowahoji kwa saa kadhaa kabla ya kufukuza nchini humo.
Umoja wa Imarati za Kiarabu ulijibu mashambulizi kwa kuongeza masharti ya visa - na kusema raia wa Kenya wenye shahada ya chuo kikuu pekee ndiyo wataruhusiwa kuingia nchini humo.
Marufuku
Marufuku huyo iliwaathiri wafanyabiashara wengi, ambao kwa kawaida hununua bidhaa zao kutoka Dubai.
Magari yaliyotumika na nguo ni baadhi ya bidhaa zinazosafirishwa kwa kiasi kikubwa kutoka Dubai kuingia Kenya.
Waziri wa mambo ya nje, Bw Wetangula na ujumbe wake waliwasili Dubai siku ya Jumatatu, lakini mazungumzo hayakuzaa matunda, badala yake muda wa majadiliano ukaongezwa.
Juma lililopita, naibu waziri wa mambo ya nje, Richard Onyonka aliomba radhi kupitia matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC kwamba maafisa husika walifanya makosa

UM yakubaliana kuwadhibiti maharamia


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa uwingi wa kura azimio linalokusudiwa kurahisisha kuwafungulia mashtaka maharamia watakaokamatwa katika pwani ya Somalia.
Rasimu ya azimio iliyoandaliwa na Urusi inatoa wito kwa mfumo wa sheria wa kimataifa kuimarisha mbinu za kukabiliana vitendo vya kiharamia.
Waraka huo unazisihi nchi zote kuunda sheria zinazopiga marufuku vitendo vya uharamia wa kuteka meli.
Maharamia waliokamatwa na majeshi ya majini ya kimataifa yanayolinda doria katika pwani ya Somalia, wamekuwa wakikabidhiwa kwa serikali za Kenya na Ushelisheli waweze kushughulikiwa kisheria.
Hata hivyo, kuna wasi wasi kwamba mfumo wa sheria wa Kenya umeelemewa na matatizo hayo.
Baadhi ya maharamia waliokamatwa wameachiliwa kwasababu ya utata wa kisheria kujua ni jinsi gani ya kuwafungulia mashtaka na kuendesha kesi zao.
Mahakama ya kimataifa
Azimio hilo linapendekeza Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, azingatie njia nyingine za kuwashughulikia na kuwafunga maharamia hao.
Hatua hizo ni pamoja na kuunda mahakama za kanda au kimataifa, au uwezekano wa mataifa kuanzisha mahakama zitakazoshirikiana na vitengo vya kimataifa.

Uchaguzi wa Sudan waendelea kuzua utata


Kiongozi wa chama cha upinzani cha pili kwa ukubwa huko Sudan Kusini ameieleza BBC kuwa kulikuwa na vitendo vingi vya ukiukwaji wa sheria katika uchaguzi wa kihistoria uliofanyika hivi karibuni.
Lam Akol, mkuu wa SPLM-Democratic Change, na viongozi wa vyama vingine vinane vya Sudan Kusini wameamua kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi.
Kiongozi wa upinzani Sudan Kusini, Lam AkolSalvir Kiir, kiongozi wa chama cha Sudan People's Liberation Movement (SPLM), alipata ushindi wa asilimia 93 ya kura zote za kusini.
Mpinzani wake pekee alikuwa Bw Akol - ambaye anachukuliwa kuwa anawakilisha maslahi ya serikali kuu ya Sudan Kaskazini.
Malalamiko
Bw Akol alimweleza mwandishi wa BBC, James Copnall, mjini Khartoum kuwa anataka mahakama zibatilishe na kutengua matokeo ya kusini kwasababu uchaguzi ulitawaliwa na udanganyifu na kwamba matokeo hayo hayawakilishi maoni ya wananchi.
"Ukweli uko wazi kabisa," alieleza.
"Mgombea [Bw Kiir] kupata asilimia 93 ya kura ni jambo halijawahi kutokea katika mchakato wa kidemokrasia.
"Pia ni ushahidi kuwa kuna udanganyifu mkubwa."
Bw Akol alidai kuwa wakati wa upigaji kura majeshi ya usalama ya SPLM yalichukua udhibiti wa vituo vya kupigia kura, waliwatisha na kuwanyanyasa wapiga kura, na kukamata wawakilishi wa vyama vya upinzani.

Tuesday, April 27, 2010

Stars United ndani Boston


Juu na chini Mpwa akiongea na wachezaji wa Stars wakati wa mapumziko

David Beckham anapendelea watoto wake wajekua wachezaji wa kabumbu

Matt Damon anategemea kupata mtoto wa tatu

Matt Damon Is Expecting Baby Number 3!
 Damon amethibitisha leo kwamba mke wake Luciana ni mjamzito,VIJIMAMBO inakupongeza

KWA MENYU HII AMAVUBI HAWATOKII!!


Kutoka kushoto ni Jabir Aziz, Yusuf Soka, Nahodha wa Stars Shedrack Nsajigwa ‘Fuso’ na Kigi Makasy wakipata msosi.
Beki wa kushoto wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Juma Jabu ‘JJ’ akipata msosi wa mchana hotelini hapo .
Beki wa kulia wa Stars Salumu Kanoni (kushoto) akiwa na Uhuru Selemani wakati wa 'Lunch' hotelini The Atriums.
Basi la Stars likiwa limepaki ndani ya hotel ya The Atriums likisubili wachezaji kabla ya kwenda mazoezini