ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 31, 2010

Balozi Sefue aagwa rasmi na wafanyakazi wa ubalozi Washington,DC


Balozi Sefue akiwa ndio amewasili
Balozi Sefue akipata menyu
Mama Mnanka akisoma lisala kwa niaba ya wafanyakazi wa Ubalozi
Mama Mnanka akimkabidhi zawadi Balozi Sefue
Manae Balozi Sefue akipokea zawadi kwa niaba ya Mama ambaye hakuwepo kwa sababu yupo Tanzania kwa shughuli za kifamilia
Balozi Sefue akiwashukuru wafanyakazi wa ubalozi 
Mpwa akijipendelea na U-Kodak na Mh:Balozi
Wadau kutoka OHio nao hawakua mbali kwenye U-kodak
Juu ni wafanyakazi wa ubalozi.chini ni wafanyakazi wa ubalozi wakiwa na familia zao
Chef Benja akiwa kazini
Chef Ally nae hakua mbali
Menyu ikiwa ready kwa mlaji
wafanyakazi wa ubalozi na ndugu  na jamaa wakiwa kwenye menyu 

Dk. Slaa awataka Duni, Hamad Rashid wa CUF

Mazungumzo ya siri yaanza Dar, Zanzibar

Aaga Karatu, atoa sababu nzito za kujitosa

BAADA ya mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ), Dk. Wilbrod Slaa, kubadili upepo wa kisiasa nchini kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, chama hicho sasa kimo katika mkakati mahususi wa kumpata mgombea mwenza mwenye ushawishi mkubwa kutoka Chama cha Wananchi (CUF), Raia Mwema limethibitishiwa.
Habari za uhakika kutoka CHADEMA na CUF zimethibitisha kwamba mazungumzo yasiyo rasmi yamekwisha kuanza pamoja na kuwa tayari majina mazito ya wanasiasa kutoka Zanzibar yameanza kutajwa kuombwa kuwa pamoja na Dk. Slaa katika uchaguzi huo wa Oktoba 31.
kwa habari zaidi Bofya hapa

Mishumaa ya Man Parrish ilikua balaa

Mshumaa wa Break Dance

Mkiwa na pesa au hamna ni wajibu wenu kudumisha penzi

Pesa inawezekana si kila kitu, pia inaweza isiwe chochote. Hata hivyo ndiyo inayotusaidia kuishi pamoja na kufanya mambo mengine yenye kufurahisha na anasa mbalimbali. Unapojumuika na unayempenda huku mfuko ukiwa umenona, ni furaha iliyoje! Fedha hutupa nguvu na kujiamini katika kutekeleza njozi na matarajio.

Mafanikio yoyote nyuma yake huwa kuna kionjo cha fedha! Zinaheshimiwa kwa sababu zina nguvu! Wapendanao wengi waliachana baada ya mmoja kuingiwa na tamaa ya kutaka zaidi ya kile anachokipata kutoka kwa mwenzi wake. Binadamu wote wangekuwa na uwezo sawa, uaminifu ungekuwa na kiwango cha juu, na neno “penzi la kweli” lingeleta maana.

Pesa imesababisha siku hizi mapenzi yasiwe na nguvu pale kwenye ukata. Wengine wamekuwa na woga wa kujishughulisha na aina fulani ya watu, kwa kuona kwamba wenye pesa wakiamua, watawanyang’anya. “Mimi mwanamke mzuri simtaki, uwezo wangu mdogo, nitanyang’anywa!” Ni kauli ya unyonge na inaumiza!

Ukweli ni kwamba palipo na mgogoro wa pesa, salio halitoshi na madeni kuongezeka, husababisha athari hasi kwenye uhusiano wako wa kimapenzi! Haijalishi ni kwa kiasi gani wewe ni mwenzako mnapendana. Ni mabadiliko ambayo hayaepukiki na wapenzi wengi yalipowafika, walipena mkono wa kwa heri bila kupenda.

Hii ni kwa sababu unapotoka kwenye maisha ya utulivu, yaliyojaa starehe, kwenda kwenye mabadiliko ya kiuchumi ambayo kila mmoja huwa hapendi itokee, husababisha msongo wa mawazo kwa wahusika na kuchochea uvumilivu ukome haraka. Hivyo basi, penzi huingia mdudu kabla ya kuwa mwanzo wa kutengana.

Inapotokea kwamba kiwango cha uvumilivu kimekuwa finyu kwa wawili wanaopendana, husababisha maudhi ya hapa na pale, kero zisizo na maelezo ya kutosha kutokana na shaka ambayo hutawala fikra za kila mmoja kwenye uhusiano. 

Je, unayo imani kwamba tatizo la fedha linaweza kuharibu muungano wako wa kimahaba na mwenzio? Inawezekana lakini siyo kihivyo! Kwa migogoro yote ya pesa uliyonayo leo, haitofautiani na ile ambayo itakufika siku za usoni au mbeleni. Maumivu ni ya wawili, ni vizuri kuvumiliana, kushikamana ili kuvuka vizingiti.

Kitu muhimu cha kufanya ni kushirikiana, kuepuka kugeukana na kucheza mchezo wa lawama. Huyu amuone mwenzake ndiyo chanzo cha tatizo. Zingatio ni kwamba mapenzi yakishamiri, kwa kiasi fulani hupunguza mawazo yanayosababishwa na ukata.

Hali imekuwa mbaya, ni sawa ila zingatia kuwa vyovyote mnavyojikuta mpo kwenye mazingira tata kiuchumi, mnapaswa kushirikiana mpaka pale yatakaponyooka. Hii inajumlisha kupanga bajeti ya vitu na kujibana kuliko mwanzo, pia kujitahidi kutafuta bidhaa za gharama nafuu, yote hiyo ni ili mfurahie maisha licha ya ukata unaowakabili.

Kushirikiana katika kutafuta vitu vyenye sura ya kimahaba, kutoka ‘out’ kwenye maeneo ambayo hayagharimu pesa nyingi, ni muhimu mno katika kuweka hai uhusiano wako, pale unapobeba tafsiri ya “mambo magumu.”

Ni aibu kizuizi cha pesa kusababisha mtengane. Ni muhimu mambo ya fedha yakapata kujadiliwa na ninyi wote pamoja. Ila mtikisiko huo hauruhusiwi kuwafanya muwe wazembe kujenga penzi endelevu. Ikitokea ni dhambi kubwa! Hamna fedha, lakini yapo mambo ambayo mkiyafanya mtafurahi, ingawa hayatogusa mfuko wa yeyote kati yenu.

Mfano, kukaa nyumbani na kuangalia muvi nzuri itawagharimu kiasi gani? Fikiria kwamba wewe na yeye mmeketi vizuri kitini sebuleni, mnazungumza mambo yenye kuleta mwanga wa kimaisha, huku matukio ya filamu yakiteka hisia zenu.

Maisha yametofautiana, inawezekana ‘cha kuonea’ hakipo nyumbani, lakini hiyo siyo ishu! Kila mtu anahitaji kupewa elimu ya mapenzi, iwe mjini au kijijini. Kwa maana hiyo, anaweza kuketi faragha na mwenzi wake na kusimuliana hadithi za kimapenzi.

Yapo mazingira mazuri yenye hewa safi, fukwe mbalimbali, bustani na kadhalika. Yote hayo ni maeneo ambayo unapaswa kuyatumia na mwenzi wako kuhakikisha furaha haipotei. Lingine ambalo linaweza kufanyika bila kuwagharimu kutoboka mifuko ni kupika chakula kizuri cha usiku ambacho kitakupendeza wewe na mwenzi wako.

Furaha kidogo huyeyusha maudhi na msongo wa mawazo! Kula ‘msosi’ mtamu, kuchombezana kwa hadithi za hapa na pale ni kitu maalum sana. Inawezekana pia, kutoka ‘out’ na kwenda kujumuika pamoja kiwanja tulivu, kupata ‘dinner’ pamoja, huku mkiburudishwa na muziki laini.

Kuna mambo mengi ya kufanya, ila pointi ya msingi ni kuwa makini na uhusiano wako na kuhakikisha huyumbishwi na matatizo ya kifedha. Hustahili kuchachawa, kuna wakati wa kupigana kwa ajili ya pesa lakini pia kipo kipindi cha kudumisha penzi.

Hisia zako kwenye pesa na mapenzi ni muhimu lakini si busara kuchanganya moja kwa lingine. Wiki ijayo tutaendelea na dondoo muhimu zitakazokuwezesha kukamilisha furaha yako ya kimapenzi wakati mambo ya kifedha yanapokwenda ndivyo sivyo.
Itaendelea wiki ijayo...


CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS

Kujichana kwa nafasi!!

Baraka Kifaru alikutwa anapata lunch ya usiku ijumaa July 30,Swahili Village

Kapitali watiwa kiwewe na Professor Jay,Swahili Village,Beltsville,MD,palikua hapatoshi









Friday, July 30, 2010

Nyama Choma Ya Besidei kwenye secret location kufika kwake mpaka uwe na Code???


Nyama choma kwenye secret location bahati mbaya u-kodak wa VIJIMAMBO ulikua chonjo na kudaka secret code

Watatu watuhumiwa na shambulio la Uganda

Watuhumiwa wa shambulio la Uganda
Wakenya watatu wameshtakiwa kwa mauaji ya watu 76 waliouliwa wakati mabomu yalipolipuka walipokuwa wakitazama fainali ya Kombe la Dunia kupitia televisheni mjini Kampala, Uganda.
Hussein Hassan Agad, mwenye umri wa miaka 27, Mohamed Adan Abdow, 25 na Idris Magondu, 42, nao walishtakiwa kwa ugaidi na mashtaka 10 ya jaribio la mauaji.
Bado hawajajitetea na wataendelea kubaki kizuizini mpaka wafikishwe tena mahakamani Agosti 27.
Al-Shabab, kundi la wapiganaji la kisomali, lilisema lilihusika na mashambulio hayo.
Majeshi ya kutunza amani ya Uganda yapo Somalia, kusaidia serikali dhaifu, inayoungwa mkono na umoja wa mataifa dhidi ya al-Shabab, yenye uhusiano na al-Qaeda.
Umoja wa Afrika wiki hii iliahidi kuongeza majeshi ya kutunza amani Somalia kufikia majeshi 4,000, baada ya mkutano uliofanyika Kampala, mji uliokumbwa na mashambulio.
Mpaka sasa ni Uganda na Burundi tu ndizo zilizopeleka majeshi yake katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu na al-Shabab ilitishia kushambulia nchi zote mbili.

'Mhubiri wa Kiislamu'

Majeruhi wakipatiwa tiba wakati wa shambulio la Kampala
Milipuko ya Julai 11, ambayo pia iliwajeruhi watu 70, iliharibu kabisa klabu ya raga na mgahawa wa Kiethiopia wakati mashabiki wa soka walipokuwa wakitazama dakika za mwisho za fainali ya Kombe la Dunia.
Watu hao, wote wakiwa raia wa Kenya, walifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi siku ya Ijumaa mjini Kampala.
Karatasi ya mashtaka imemwelezea Hussein Hassan Agad kuwa "mhubiri wa kiislamu", huku Idris Magondu akiwa mfanyakazi wa kampuni moja mjini Nairobi, Kenya.
Watu hao walishtakiwa kwa makosa 89. Wanakabiliwa na makosa ya mauaji ya watu 61 kwa wale waliouliwa kwenye klabu ya raga ya Kyadondo na makosa 15 kwa wale waliouliwa kwenye mgahawa wa raia wa Ethiopia.
Mashtaka hayo pia yanajumuisha makosa matatu ya ugaidi na makosa 10 ya jaribio la mauaji.
Watu hao hawakuzungumza lolote walipofikishwa mahakamani.
Mwandishi wa BBC Ignatius Bahizi, aliyekuwa mahakamani, alisema watu hao walikamatwa Julai 12, siku moja baada ya mashambulio hayo.
Alisema, kulikuwa hamna ishara yeyote ya muda gani walikuwepo Uganda kabla ya mashambulio hayo.
Alisema takriban watu 27 walikamatwa na timu ya wachunguzi ya kimataifa, ikiwemo shirika la kijasusi la Marekani FBI.
Polisi wamesema watawafikisha washukiwa zaidi mahakamani katika siku za usoni.