Tuesday, January 11, 2011

CRDB yakiri kuitaifisha Sekondari kufidia deni

Hemed Athuman (TSJ) 
BENKI ya CRDB imekiri kuichukuwa Shule ya Sekondari ya Mkandawile  kwa   kufidia mkopo wake walioutoa kwa mmiliki wa shule hiyo.

Ofisa uhusiano wa benki hiyo aliyejulikana kwa jina la Manel alisema shule hiyo kwa sasa ipo chini ya benki ya CRDB, lakini hawezi kuongelea lolote kuhusu shule hiyo kwa sababu taratibu zote ziko chini ya Bodi ya wakurugenzi.


Inadaiwa mmiliki wa shule hiyo anadaiwa zaidi ya Sh 500 milioni.
“Siwezi kuongelea chochote kile kuhusu suala la Shule ya Mkandawile kwa sababu mkurugenzi mkuu hajazungumzia lolote  kuhusiana na shule hiyo,”alisema Manel.

 Shule ya Mkandawile iliyopo Majohe,  Kata ya Chanika Wilaya ya Ilala ilichukuliwa na Benki ya CRDB  tangu  Oktoba mwaka jana,  ambapo wanafunzi pamoja na walimu waliachwa kuachwa njiapanda bila ya kujua la kufanya.

 Hii ni wiki ya tatu sasa, baadhi ya walimu wa shule hiyo walihamishia makazi yao kwa  aliyekuwa mmiliki wa shule  Alfan Mkandawile ambaye naye baada ya shule hiyo kutokuwa mikononi mwake aliamua kutokomea kusikojulikana.

Walimu wa shule hiyo, akiwemo Kaimu Mkuu wa Shule, Michael Sigore kwa nyakati tofauti walilidokeza  gazeti hili kuwa wamdai kiongozi wa shule  mishahara ya miezi saba na kwamba  wenye nyumba walikopanga wamewafukuza ndio maana  wamehamishia familia zao kwa Mkandawile
                                                  Chanzo:Mwananchi

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake