Flaviana Matata akiwa na Russell Simmons.
Na Musa Mateja
Miss Universe 2007-08, Flaviana Matata ameamua kufunua kinywa na kueleza kwamba hajawahi kutoa penzi kwa tajiri wa Marekani, Russell Simmons, 53.
Flaviana alisema, Simmons ni bosi wake kupitia kampuni yake kubwa ya mavazi nchini Marekani lakini wambeya wanazusha kwamba wanatoka kimapenzi.

‘The Biggest IQ’, Ijumaa Wikienda lilikutana na Flaviana kwenye Klabu ya Runaway, Shoppers Plaza, Dar es Salaam na lilipomuuliza kuhusu shemeji yetu babu Simmons, alijibu:
“Sina ruhusa ya kufanya intavyuu na waandishi bila mawasiliano na meneja wangu lakini kwa ufupi Russell Simmons ni bosi wangu na wanaoeneza uvumi huo wanatakiwa waelewe hivyo.”
Aliendelea kusema kuwa ameona habari ya yeye kutoka na Simmons ipo kwenye mitandao mingi, wakati ni ya uongo.
“Nalazimika kuongea hivyo kwa sababu watu wanahusisha mambo wasiyoyafahamu na kuyavalia njuga bila ufafanuzi wowote kutoka kwa mhusika. Mimi ndiye mhusika, siyo kweli na nadhani niishie hapo,” alisema Flaviana.
Moja ya ishu zilizovuma mwaka jana kwenye ulingo wa burudani ni Flaviana kudaiwa kutoka kimapenzi na Simmons.
Flaviana aliyeingia Sita Bora kwenye mashindano ya dunia ya Miss Universe mwaka 2007, kwa sasa anajishughulisha na masuala ya mitindo nchini Marekani, akitangaza mavazi ya Kampuni za Simmons, Phat Farm, Argyleculture na American Classics.

CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake