POLISI mkoani Singida wamemkamata mkazi wa Musoma mkoani Mara, Robert Mbaga (36) kwa tuhuma za wizi wa gari jipya aina ya Noah.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Nyigesa Wankyo, amesema jana kuwa, mtuhumiwa huyo aliiba gari hilo lenye rangi ya fedha na chesisi namba SR400183787 eneo la Kawe, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamanda Wankyo, tukio hilo lilitokea Januari 15 saa 8 mchana baada ya mtuhumiwa kutumia funguo bandia na kuliiba gari hilo.
Wankyo amesema, kutokana na taarifa za Jeshi hilo kuwafikia mapema, Polisi mkoani Singida waliweka mtego na Januari 19 saa 5 asubuhi, mtuhumiwa alitiwa mbaroni akiwa na gari hilo.
"Tulipomhoji kuhusu gari hilo, Robert alidai amelinunua; lakini alipotakiwa kuonesha stakabadhi ya manunuzi hakufanya hivyo," alisema Kaimu Kamanda na kuongeza kuwa mtuhumiwa atasafirishwa hadi Dar es Salaam ili kujibu mashitaka.
Wakati huo huo, Jeshi hilo limekamata wakulima wawili wakazi wa kijiji cha Kipuma, Singida Vijijini, kwa tuhuma za kumiliki silaha aina ya gobori bila uhalali. Tukio hilo lilitokea Januari 19 saa 4:30 asubuhi.
Watuhumiwa hao Iddi Mohamed ( 55 ) na Ramadhan Iddi ( 29 ) wote wakazi wa Kipuma.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake