MTOTO Baraka Bahati Rose (14), (pichani) aliyeishi na nyani porini kwa kipindi cha miaka mitano na kuokolewa na maofisa wanyama pori, amebadilika na sasa anaonesha maajabu katika kusakata soka na pia kufanya vizuri darasani.
Mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Kimanga, Wilayani Ilala jijini Dar es Salaam aliyejitambulisha kwa jina la Christina, aliliambia gazeti hili wiki iliyopita kuwa Baraka amekuwa akifanya vizuri na kucheza mpira kitaalamu zaidi, hali inayomfanya apendwe na walimu na wanafunzi.
“Baraka anajitahidi sana na siyo katika masomo tu bali hata katika mchezo wa mpira wa miguu, ni staa na anapenda kujisomea, amekuwa akifanya vizuri sana hasa katika masomo ya Sayansi,” alisema Mwalimu Christina.

Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo waliliambia gazeti hili kwamba, Baraka ambaye yupo Darasa la Nne kwa sasa amebadilika kwa asilimia kubwa katika masomo ya Sayansi na amekuwa akicheza mpira wa miguu vizuri kuliko wenzake.
“Tunapocheza mpira wa miguu na kuchagua timu, kila mtu anapenda awe katika timu yake,” alisema mtoto mmoja wa kiume aliyejitambulisha kwa jina la Said.
Wanafunzi hao walisema kuwa Baraka amekuwa akiwapenda wenzake tofauti na awali ambapo alikuwa haongei vizuri Kiswahili na hakuwa na uhusiano mzuri na wanafunzi wengine.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimanga, Pastor Kyombia kwa kushirikiana na mlezi wa Baraka aitwaye Rose Mbwambo wamekuwa wakimtunza mtoto huyo.
Chanzo:Global Publishers
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake