Sunday, January 9, 2011

Sudan ya kusini yapiga kura-BBC Swahili

Wapiga kura Kusini mwa Sudan wamejitokeza kwa wingi kupiga kura ya maoni itakayosababisha Sudan Kusini kuwa nchi huru na jipya kabisa kote duniani.
Maelfu ya wapiga kura wakipiga foleni
Maelfu ya wapiga kura wakipiga foleni
Maelfu ya wapiga kura walipiga foleni katika vituo vya kupiga kura hata kabla ya vituo hivyo kufunguliwa.

Rais wa Sudan ya kusini, Salva Kiir, alikuwa miongoni wa waliotangulia mapema kupiga kura.
Rais wa Sudan ya kusini, Salva Kiir
Rais wa Sudan ya kusini, Salva Kiir
Raia wa Kusini wanaoishi kaskazini mwa Sudan nao pia watapiga kura lakini hakuna shamrashamra za kisiasa kama ilivyo Sudan ya Kusini.
Wengi wameyahama makazi yao kaskazini kurejea eneo la mababu zao ambayo ni Sudan Kusini.
Lakini baadhi ya raia wa kusini mwa Sudan wameelezea wasiwasi kuhusu mustakabali wao ikiwa Sudan ya kusini itajitenga.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake