*AKAGUA MITAMBO YA DOWANS KINYEMELA
WINGU zito lililokuwa limetanda kuhusu picha ya mwanahisa mkubwa wa Kampuni ya Dowans, Brigedia Jenerali Mohammed Yahya Al Adawi, limeyeyuka baada ya kunaswa jana kwenye mtego wa kamera wakati alipotembelea mitambo ya kampuni hiyo iliyopo Ubungo jijini Dar es Salaam.
Jenerali Al Adawi ameibua mjadala mzito nchini tangu alipotua na kufanya mkutano na wahariri wa magazeti matano Jumapili iliyopita, akigoma kupigwa picha pia akizuia televisheni na redio, huku akificha sura yake na sauti.Hata hivyo, mbio hizo za Al Adawi kukwepa kamera za waandishi jana ziliishia ukingoni baada ya kunaswa na gazeti hili akikagua mali zake zilizopo Ubungo.
Mpango mkakati wa kumnasa Al Adawi, ulipangwa na kufanikishwa kwa pamoja na duru huru za habari kutoka kwa raia wema ambao, awali walidokeza kuwa bosi huyo wa Dowans angefanya ziara kukagua mitambo ya kampuni hiyo mapema asubuhi.
Hata hivyo, mwanajeshi huyo mstaafu wa Jeshi la Oman, ratiba yake haikuwa wazi kwani duru nyingine za habari zilieleza Mwananchi kuwa, angewasili eneo hilo saa 7:00 mchana badala ya asubuhi.“Sina uhakika na ujio wa mtu huyo, lakini kwa taarifa zisizo rasmi mgeni huyo anaweza kuingia eneo hili saa 7:00 mchana. Labda kama utafika muda huo unaweza kufanikiwa kumuona, lakini sina uhakika," kilifafanua chanzo kimoja cha habari.
Lakini, kama wahenga walivyosema subira huvuta heri na hakuna marefu yasiyo na ncha, baada ya subira ya muda mrefu, bosi huyo wa Dowans alifika kwenye mitambo ya kufua umeme wa dharura saa 8:20 mchana akiongozana na watu watatu, ambao haikufahamika mara moja iwapo walikuwa wafanyakazi wa Tanesco au Dowans na kutumia dakika 22 kwenye ziara hiyo.Watu hao walifanya kazi ya kumuongoza Al Adawi kwenye maeneo ilipo mitambo hiyo, huku gazeti hili likishuhudia mmoja wao akimuonyesha bosi huyo mahali ilipo mitambo ya Dowans.
Akiwa ndani ya eneo hilo la Tanesco, bosi huyo alifanya ziara kwa dakika hizo, huku kila alipotembelea wafanyakazi walionyesha utiifu wa hali ya juu.Pia, Mwananchi ilishuhudia mmoja kati ya watu watatu alioongozana nao, akimuelekeza na kumuonyesha mitambo hiyo.
Akiwa eneo hilo, Mwananchi ilifanya mahojiano na baadhi ya wafanyakazi waliokuwamo ndani na kuelezwa kuwa, wao hawamfahamu mtu huyo ndio mara yao ya kwanza kumuona.“Mimi simfahamu kabisa mtu huyo isipokuwa nimeshangaa kuona mabosi wangu wote wakielekea huku juu aliko, kisha baadhi yao kuongozana naye,”alisema mmoja wa wafanyakazi ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe kwa sababu za usalama.
Mwananchi ilishudia pia kila alipokuwa akipita Al Adawi, walinzi na wafanyakazi wengine waliokuwapo walisimama kuonyesha heshima hadi bosi huyo alipopita eneo hilo, ndipo walipokaa chini na kuendelea na shughuli zao za kawaida.
Hali hiyo ilimsukuma mwandishi wa habari hizi kufuatilia na kuwauliza baadhi ya walinzi, iwapo wanamfahamu mtu huyo, lakini akajibiwa, "Hatumujui, lakini, ameongozana na baadhi ya mabosi wetu ndio sababu tunasimama kutoa heshima.”Al Adawi ni mmoja wa watu ambao majina yao yako kwa Wakala wa Usajili wa Kampuni nchini (Brela), waliojiandikisha kama wamiliki wa kampuni hiyo ya Dowans.
Watu wengine waliotajwa na Brela kuwa ni wamiliki wa Dowans Tanzania Ltd, ni Dowans Holding S.A, Costa Rica na Portek Systems and Equipment (PTE) Ltd na uraia wao kwenye mabano ni Andrew James Tice na Guy Picard (Canada), Gopalakrishnan Balachandaran (India), Stanley Munai (Kenya) na Hon Sung Woo (Singapore).
Ujio wa Al Adawi ulitajwa kama njia pekee ya kuja kuweka mambo sawa, huku naye akisema yuko tayari kuzungumza na Tanesco kuhusu fidia ya Sh94 bilioni (hakutaja kiasi), baada ya kuvunjwa kwa mkataba baina ya kampuni yake hiyo na Tanesco."Nimekuja kwa mambo mawili; moja ni kuondoa sintofahamu iliyopo hivi sasa kuhusu Kampuni ya Dowans na kuangalia kama kuna uwezekano wa kuwapo suluhisho la kile kilichopo hivi sasa kuhusu Dowans," alisema Al Adawi.
Lakini Al Adawi ambaye katika mkutano huo aliambatana na mwanasheria wa kimataifa, John Miles na Mkurugenzi wa Fedha, Stanley Munai wa Dowans Tanzania Ltd, alisema licha ya Tanzania kuwa kivutio cha uwekezaji, kampuni yake nchini imekumbwa na jinamizi kwenye uwekezaji.“Nimekuwa na imani na Tanzania na nimeitikia wito wa uwekezaji kipindi cha matatizo yenu, lakini yote yaliyojitokeza tangu niwekeze nchini ni unyanyasaji na mnaendelea kuninyanyasa hadi leo na katika hali ya kawaida hamnitendei haki," alisema Al Adawi.
Mfanyabiashara huyo alieleza kuwa, hakuwa ametaka kuishtaki Tanesco na kudai fidia ya mabilioni hayo ya shilingi, lakini amelazimika kufanya hivyo kutokana na jinsi alivyotendewa kipindi cha uwekezaji wake.
Al Adawi alifafanua kuwa Tanesco ilimhakikishia usalama wa uwekezaji wake,hivyo akakubali kuingia nao mkataba, lakini shirika hilo likavunja mkataba huo na kukiuka makubaliano yaliyofikiwa chini ya sheria zake zenyewe za ununuzi.
CHANZO NA PICHA: MWANANCHI

1 comment:
Kwa kweli to tell the truth kama watanzania tunavyosema kuzulumiwa sio kuuzuri sasa mie nnasema/nnaona huyu jaama alijitokea kwa moyo kuja kuisaidi tanesco then hapahapa wao tanesco ndo wamevunja mkataba then suala tulaumu nani???hata mtoto ndogo anaweza jibu hilo PUT YOUR SELF INTO HIS SHOES kama mfanyabiashara yeye wala hana makosa ni hao watendaji huko tanesco walikua sio makini.So ninachosema HEBU TUNDETEHE HAKI JAAMA NA SIO YEYE TU HATA WENGINE COS SASA WAWEKEZADI WATAIOGOPA TZ hayo ndo mawazo yangu binasfi.....MEYA SEATTLE........A-DOLA
Post a Comment