ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 22, 2011

RISASI ZA MOTO NA MABOMU YARINDIMA ARUSHA-GPL

Joseph Ngilisho,Arusha
JESHI  la polisi mkoani Arusha limelazimika kuwatawanya wafuasi wa Chadema kwa kutumia risasi za moto na mabomu ya machozi.  Wafuasi hao walikuwa wakitoka mahakamani huku wakimsindikiza mbunge wa jimbo la Arusha mjini, Godbles Lema  (pichani kati) kuelekea ofisini kwake.

Vurugu hizo zilitokea punde wakati wafuasi hao wakiwa katika barabara ya Boma ambapo walipofika mkabla na ofisi ya mbunge huyo iliyopo  jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha ndipo mkuu wa polisi wilayani Arusha,Zuberi Mwombeji aliapomuru polisi kufyatua  mabomu na risasi za moto angani kitendo kilichofamya wafuasi hao kutawanyaika huku mbunge Lema akikimbilia ofisini kwake.

Wafanyabiashara waliokuwa karibu na eneo hilo walionekana wakifunga maduka huku ofisi za manispaa ya Arusha na watu waliokuwa ndani ya jesngo la ofisi ya mkuu wa mkoa wakitoka nje ya jengo hilo kushuhudia vurugu hizo huku polisi waliokuwa kwenye magari mawili aina ya defender moja lenye namabri PT 1844 wakijitahidi kuwatawanya wafuasi hao .

kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha, Akili Mpwapwa alipoulizwa juu ya tukio hilo alishindwa kukiri wala kukataa juu ya tukio hilo lakini alidai  kuwa ofisi yake bado inafuatilia tukio hilo kwa kina na atatoa taarifa kamili baadaye.

No comments: