Sunday, March 13, 2011

10,000 wahofiwa kufariki dunia Japan.BBC

Kazi za uokozi zinaendelea na katika eneo moja lilopigwa na tsunami, inahofiwa watu kama elfu kumi wamekufa.
Juhudi za ukombozi Japan
Juhudi za ukombozi Japan
Wakuu wa Japani wameonya kwamba kunaweza kutokea mripuko mwingine kwenye kinu cha nishati cha nuklia kaskazini ya mji wa Tokyo, wakijaribu kuzuwia tanuri ndani ya kinu, kuripuka.

Wamekiri kuwa miyale ya nuklia karibu na kinu hicho kilioko Fukushima wakati mmoja ilizidi kiwango kinachofikiriwa kuwa salama baada ya kinu hicho kuharibika katika tetemeko kubwa lilotokea Ijumaa.
Wahandisi wamejaribu na kushindwa kupooza tanuri katika kinu kimoja kwa kutumia maji ya chumvi.
Lakini wanafikiri pipa linalofunika tanuri ni imara na litahimili mripuko kwa hivyo miyale haitovuja.
Jana kulitokea mripuko mkubwa kwenye kinu kimoja cha Fukushima.
Jeshi likitoa msaada wa dharura kwa raia wa Japan
Jeshi likitoa msaada wa dharura kwa raia wa Japan

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake