Tuesday, March 15, 2011

Auawa akimuokoa mwanamke

Na Haruni Sanchawa
Katika hali ya kushangaza, kijana mmoja, Mohamed Ahmed Lwambano amepigwa ngumi na mtu ambaye hajajulikana na kufa papo hapo wakati akijaribu kumuokoa mwanamke aliyeanguka ghafla katika kituo cha mabasi cha Gongo la Mboto mwishoni mwa wiki iliyopita.

 Tukio hilo la kusikitisha lilitokea majira ya saa 11 jioni ambapo kijana huyo alijaribu kuokoa begi la mama huyo ambaye baada ya muda mfupi aliaga dunia. Hadi wakati gazeti hili linaondoka eneo la tukio, mama huyo hakuweza kufahamika jina wala sehemu anayoishi.


Mashuhuda waliliambia gazeti hili kuwa, kabla mwanamke huyo hajafikwa na mauti, alikuwa amesimama kituoni hapo huku akionekana kutokwa na jasho jingi. Muda mfupi baadaye alianguka, watu wakamzunguka na kuanza  kumpepea.

Habari zinaeleza kuwa, baada ya mama huyo kudondoka chini, Lwambano alijitokeza kwa kwa lengo kumsaidia lakini ghafla alijitokeza kijana ambaye hakujulikana na kumpiga (Lwambano) ngumi moja ya utosini, akadondoka chini na kufa.
Baadaye polisi waliitwa na kuichukua miili yote miwili, wakaipeleka Hospitali ya Amana kuhifadhiwa.
Taarifa kutoka kwa familia ya Lwambano zinadai kuwa, ilikuwa ni wiki moja tu tangu ndugu yao huyo alipofiwa na mdogo wake huko Songea. Inazidi kuelezwa kuwa, siku hiyo Lwambano alikuwa amevaa nguo za marehemu kwa madai kuwa alifanya vile kumuenzi nduguye.

Wakati huo huo, mkazi wa Buza kwa Kidagaa wilayani Temeke, alikutwa amejinyonga hadi kufa kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ugumu wa maisha na wivu wa kimapenzi.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa, Ally Salim (48), maarufu kwa jina la Kidevu (pichani) aliyekuwa fundi mwashi, alimpigia simu  mdogo wake kumpa maelekezo ya mahali atakapozikuta simu yake na ya mkewe. Pia aliamuaga kuwa anaenda makaburini bila kueleza sababu inayomfanya aende huko lakini alipofika kwake akakuta amejinyonga
Akizungumza na gazeti hili, mke wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Hadija Ismail alisema kuwa mumewe hakuwahi kumsikia akilalamikia jambo lolote hivyo kushangazwa na hatua yake ya kujinyonga.
Hata hivyo, watu wa karibu wa marehemu wamedai huenda kifo cha Ally kimesababishwa na ugumu wa maisha na wivu wa mapenzi kwani alikuwa ameoa wake wawili, mke mkubwa akiwa jijini Dar es Salaam na mwingine Kimbiji, Pwani.


CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake