Timu ya taifa ya vijana wa umri wa chini ya miaka 23, imeanza kwa kipigo katika mechi yao ya kuwania kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki baada ya kulala kwa magoli 2-1 ugenini Cameroon.
Kipa wa timu ya taifa, Shaaban Kado, ambaye juzi Jumamosi aliidakia timu ya taifa ya wakubwa ya Taifa Stars katika mechi ya ushindi wa 2-1 wa Kundi D la kuwania tiketi ya Mataifa ya Afrika (CAN) 2012 dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kabla ya kusafiri alfajiri ya jana kwenda Cameroon, aliiepushia timu ya vijana kipigo zaidi baada ya kudaka penalti.
Kado alisafiri alfajiri ya jana pamoja na mfungaji wa goli la ushindi katika mechi dhidi ya Afrika ya Kati, Mbwana Samatta kwa ajili ya kwenda kuiongezea nguvu timu hiyo ya vijana, ambayo sasa itasubiri mechi ya marudiano na Wacameroon hao itakayofanyika Aprili 10 jijini Dar es Salaam.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment