ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 24, 2011

Mhudumu wa mnara wa kuongozea ndege asinzia

The FAA control tower at Reagan National Airport ...
Uchunguzi unafanywa na Federal Safety Official kuhusu ripoti iliyotolewa kwa ndenge mbili zilizotua Reagan National Airport bila ya kuongozwa na mhudumu wa mnara wa kuongozea ndege uwanjani hapo.

Mtu mmoja mfanyakazi uwanjani hapo ambae hakutaka kutajwa jina,amesema mhudumu huyo alikua peke yake na ndio ilikua zamu yake wakati ule lakini alisinzia.

Msemaji wa bodi ya Usalama wa Anga,Bw.Peter Knudson amesema mkasa huu umetokea Jumanne usiku

Bw.Knudson aliendelea kwa kusema kwamba,marubani wa ndege zilizotua uwanjani hapo zilipojaribu mawasiliano na Mhudumu huyo lakini majibu yalikua kimya ndipo walipowasiliana na kitengo uongozaji cha usalama wa anga kilichopo Virginia/
Maafisa wa usalama wa aanga bado hawajasema ni hatua gani watakazo mchukulia mhudumu huyo

No comments: