Mwanafunzi wa kiume wa Shule ya Msingi Vetenari wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam amejinyonga baada ya kuadhibiwa na baba yake kwa utoro.
Mwanafunzi huyo, Idd Tajiri alikutwa amejinyonga juzi katika eneo la Kiwalani.
Marehemu alikutwa majira ya saa 12:00 asubuhi kwenye eneo la majengo ya Mamlaka ya Hali ya Hewa katika jumba bovu akiwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani.
Akielezea tukio hilo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kipolisi ya Temeke, David Misime, alisema mtoto huyo alichukua uamuzi wa kujinyonga baada ya kuadhibiwa na baba yake mzazi, Tajiri Mbegu (54), kutokana utoro shuleni.
Kamanda Misime alisema kuwa baba mzazi wa mtoto huyo alisema kuwa mwanae huyo alitoroka nyumbani tangu Machi 11, mwaka huu baada ya kumuadhibu kutokana na utoro shuleni na kumtaka kesho yake waongozane kwenda shuleni ili akaonane na walimu.
Kamanda Misime alisema kuwa baada ya baba yake kumweleza hivyo, ndipo mtoto huyo alioondoka nyumbani na baadaye juzi alikutwa akiwa amejinyonga.
Alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana na kwamba upelelezi unaendelea.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment