
Na Luqman Maloto
Katika somo lililopita, niligusia ushauri wa Brandon King na makala yake ya “Be aware with ones heart”. Nilieleza kuwa ni kosa kubwa kumuona mwenzi wako hana thamani na wakati huo huo ukatoa kipaumbele kwa watu wa pembeni.
Tafsiri inayotawala katika uhusiano ni kuwa, kundi linalosumbua na kuonekana ni sugu kwa tabia ya namna hii ni lile linalowahusisha memba wanaoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi pasipo kuwa na imani kamili.
Katika somo lililopita, niligusia ushauri wa Brandon King na makala yake ya “Be aware with ones heart”. Nilieleza kuwa ni kosa kubwa kumuona mwenzi wako hana thamani na wakati huo huo ukatoa kipaumbele kwa watu wa pembeni.
Tafsiri inayotawala katika uhusiano ni kuwa, kundi linalosumbua na kuonekana ni sugu kwa tabia ya namna hii ni lile linalowahusisha memba wanaoingia kwenye uhusiano wa kimapenzi pasipo kuwa na imani kamili.
Wanajaribu bila kuwa na ufahamu kwamba moyo haufanyiwi majaribio.
Hii ndiyo sababu ya kusisitiza kuwa, ikiwa hujaamua kupenda basi kaa mbali. Kuna mengi unayoweza kumsababishia mwenzako. Utampotezea muda huku ukimjengea imani kuwa upo naye lakini mwisho atajikuta anauguza donda la moyo. Sikitiko la mahaba linashinda msiba!
Hujaumia? Subiri usimuliwe. Moyo unapouma kwa sababu ya mapenzi hakuna kitu cha kuupoza. Unaweza kunywa pombe na usilewe, ukabugia dawa za usingizi na usilale. Kifua kitajaa kwa sababu inaathiri mfumo wa upumuaji na mapafu nayo hupata maumivu.
Sikitiko la mahaba ni hatari, likikufika utapungua uzito kwa kasi bila maelezo ya ziada. Chakula hakiwezi kupita na macho yanaweza kujaa machozi ilhali unatamani kujizuia. Binadamu tumetofautiana, wapo wanaotamani kupendwa lakini wengine wanawacheza shere wanaowapenda.
Dawa kuu ni kujihadhari na watu wasio na mapenzi ya dhati. Kuwaepuka kadiri inavyowezekana. Ni mzuri na anakuvutia lakini heri umuone kwa mbali kwa sababu ukimjaza moyoni atakusumbua. Atakutoa machozi katika eneo ambalo ulihitaji kufurahi.
Maumivu yako hatayajali kwa sababu hana hisia na wewe. Atakusaliti bila woga kwa sababu hana hofu yoyote juu yako. Itakuwa ngumu kumwacha, vilevile utaona uamuzi wowote wa kutengana naye ni mateso makubwa kwamba heri uumie ukiwa naye kuliko kuachana.
Usijidanganye ndugu yangu, wewe ni binadamu uliyekamilika. Usitarajie mtu wa pili au wa tatu anaweza kusikia kile kinachokuuma moyoni. Mateso yaliyopo ndani yako unayajua mwenyewe. Unatakiwa kuwa wa kwanza kujihurumia na kuchukua uamuzi wa kujiokoa na mateso.
Kuna kitu kimoja ambacho unatakiwa kukifahamu; binadamu ni wa ajabu sana. Hata wakiyajua mambo ya siri na kile ambacho mwenzi wako anakifanya pembeni, hawatakwambia badala yake wataketi pembeni kukuzungumzia. “Aah yule wa ajabu, anadhani kapata mpenzi kumbe kapatikana!”
Wengine utakaa nao meza moja kushauriana mambo mbalimbali lakini anayekwambia umvumilie mwenzi wako licha ya vitimbi anavyokufanyia, ndiyo huyo huyo akikaa pembeni na watu anawaambia kwa mtindo wa kukucheka kwamba unamng’ang’ania mpenzi bomu.
Lingine ni kuwa, unapokuwa na mpenzi ambaye hakuheshimu, thamani yako katika jamii inashuka. Siyo mpaka akutukane, bali vitendo vyake vitaonesha kwamba hakuheshimu. Kutoka na wapenzi wengine, kujenga mazoea ya kupitiliza na watu wa jinsia nyingine mpaka anahusishwa kutoka nao kimapenzi ni baadhi ya dalili.
Mathalan, mpenzi wako anakuwa na urafiki na watu mpaka anafikiriwa kuwa anatembea nao. Hii ni tabia mbaya na haikubaliki ingawa wapo wazuri wa kutetea. Watasema, sisi ni washkaji tu ila fahamu mapenzi yenu yanazikutanisha familia mbili. Una ndugu, marafiki na wazazi.
Inakuwaje mpenzi wako anahisiwa kutoka na mwanamke/ mwanaume mwingine na taarifa zinafika mpaka kwa wazazi wako? Watajua mkwe wao ni kicheche na hilo litakugharimu kwa kiasi kikubwa. Unatakiwa kulinda thamani, heshima na utu wako, kwa hiyo achana na mtu asiyejua maana!
Unaweza kuona leo inakuuma kwa sababu unaepukana na mtu ambaye unampenda lakini hiyo ni nafuu kwako kesho. Amini kwamba mwisho wa mateso hayo ya moyo ni furaha kubwa. Mwisho utajiuliza ni kipi kilichokuwa kinakufanya uumie kwa muda wote? Upo huru sasa!
Mapenzi maana yake ni utulivu wa moyo, yaani wewe na mtu wako spesho muogelee katika dimbwi maalum wote mkiwa na amani. Mkishirikiana katika hali zote inakuwa hakuna anayewaza la kwake peke yake isipokuwa kwa ajili yenu.
Ukilia anakuwa wa kwanza kukubembeleza, anapogundua amekuudhi ni mwepesi kukuomba msamaha. Anasoma mabadiliko yako na kukuuliza kile kinachokusumbua. Anaficha siri zako, anazungumza lugha tamu na hisia zake zote zipo kwako. Kwa wengine haoni wala hatamani.
USITHUBUTU KULAZIMISHA PENZI
Yamewafika wengi na wameumia, ni vizuri kuwa makini. Utauguza donda la moyo lisiloweza kutibika, utakonda wenzako watakucheka, atakugeuza punda afanye anachokitaka. Ni kazi bure kumpenda mtu asiyekupenda.
Pamoja na maumivu unayoweza kuyapata lakini kuna vitu hivi lazima vikukute kwa huyo mwenzi wako wa kulazimisha.
ATAKUTESA KWA UBINAFSI WAKE
Hana mapenzi ya kweli na wewe kwa hiyo si kila wakati atakufikiria. Kama hamjawa kwenye ndoa, itakusumbua kwa sababu ni ngumu kufikiria kwa ajili yenu. Atawaza kwa matilaba yake. Kama kuoana, utalazimisha wewe lakini yeye hatakuwa na habari.
Mkiwa kwenye ndoa, hatajisikia fahari kutoka na wewe, atalazimisha maisha ya kila mmoja kuwa huru kufanya mambo yake. Nguo atanunua za kwake na hata siku moja hutaona amekununulia. Wewe utafanya mengi kwa ajili yake lakini yeye atabaki na ubinafsi wake. Atakutesa, pasha moto ubongo!
AKIONA WENGINE ATAHISI NI WAZURI ZAIDI YAKO
Mtu huishi kwa fikra zake, kwa hiyo kwa sababu hakupendi kwa moyo wake wote inakuwa ngumu kukukubali. Anapokutana na watu wengine barabarani atadhani ni wazuri kuliko wewe. Atababaika hata mbele yako.
Unahitaji heshima ya kiwango cha juu. Kwa kawaida mpenzi wako anapaswa kukuona wewe ni mtu namba moja. Kama hakupi nafasi hiyo maana yake anapenda nusunusu au hapendi kabisa. Usikaribishe mateso, fikiria kesho, chukua uamuzi leo.
HASIFU MUONEKANO WAKO, ANA LAKE KICHWANI
Hujiulizi, kila siku anakuona lakini hakusifii? Ni wazi kuwa hata kama wewe ni mzuri kiasi gani, unavaa na kupendeza kwa namna bora kabisa, mwenzi wako hawezi kukupa pongezi kwa sababu ana lake kichwani.
Ukiona hilo ujue kwamba yupo mtu ambaye anamsifu kwa sababu ndiye anayemkubali na wewe utasifiwa na wengine. Inauma mwenzi wako kukuacha nyumbani na kwenda kumwaga sifa pembeni wakati na wewe unazihitaji. Una thamani kubwa, pigania utulivu wa moyo wako!
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake