Kikosi cha Simba Kikikaguliwa na Afisa Ubalozi Suleimani Saleh kulia kwake ni Mh:Mshamu Abdullah,
Afisa Ubalozi akikikagua kikosi cha Yanga
Libe Germany Defense kuongoza kikosi cha Simba,Columbus,OH
washambuliaji wa Simba kukikwaa kisiki cha Maalim,Beki mahili Yanga
Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Simba
Mechi ya watani wajaji ambayo imejichukulia umaarufu mkubwa kwa wachezaji na mashabiki wa pande zote mbili Ughaibuni,kwa mara ya kwanza mwaka huu watacheza nje ya DC.
Hii itakua ni mechi ya kwanza mwaka huu kuakutanisha mahasimu hao,mechi ya mwisho iliyochezwa Meadowbrook Park Yanga waliibuka washindi kwa kuibanjua Simba 3-2 hii mechi ililikua ya Simba kujaribu kulipa kisasi baada ya mechi yao ya kwanza mwanzoni mwaka 2010 kuambulia patupu pale ilipobanjulia bao 5-2 na mahasimu hao wa Jangwani.
Kawaida Simba na Yanga hucheza April 26 kusherehekea siku ya Muungano,mwaka huu mechi imesogezwa mbele kwa sababu kuu mbili kwanza kuwapa wachezaji muda zaidi wa kujiandaa na mtanange huu wa kukata na shoka pili kuwapa nafasi washabiki wa mikoani kushuhudia mpambano huu wa watani wa jadi
Mechi itachezwa Jumapili May 29,2011 uwanja utakaochezewa mtanange huu utatangazwa baadae,mechi ya marudiano itachezwa siku ya kuazimisha miaka 50 ya Uhuru na mechi itachezewa DC.
Pia mazoezi yataanza rasmi Jumapili hii April 3,2011,Meadobrook Park kwa wachezaji wa pande zote za Simba na Yanga kwa maandalizi ya mpambano huo
No comments:
Post a Comment