ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 23, 2011

Viongozi Tanzania ni WANASIASA ua WAPIGAPOROJO?

Na Fadhili Hezekiah
Tanzania hakuna wanasiasa,wote njaa tu na ulevi wa sifa ndo vinawasumbua! mwanasiasa ni mtu wa kuona mbali,sasa wenzangu na mimi wanataka kuingia madarakani au wapo madarakani kwa visera vyao vya miaka mitano mitano,tutafika wapi. Vi-sera vyao ukivisoma kwanza sio representative kwa mawazo na mahitaji ya watanzania wote, pili viko kama bajeti za kuendeshea kay moja tu na sio taifa!
Na ndo maana wanatuingiza katika mikataba ya kihuni isiyokuwa na tija kwa taifa,sababu hawaoni mbali,pia uwezo wao wa kufikiri na kuongoza ni wa kiwango cha familia tu na sio taifa!

Linapotokea tatizo hukurupuka na kutafuta shortcut kuficha tatizo,matokeo yake ndio hayo ya kuilipa DOWANS pesa ambazo tunazihitaji sana katika kipindi hiki,au yale ya kuanzisha bodi ya mikopo bila kujua itafanya kazi gani,wala kujua ugumu wa kazi ulivyo,wanakaa na kula pesa tu katika vikao,wakiwaacha vijana wanahangaika na masomo bila hizo pesa walizo sema watawapa. Hii ni aibu sana kwa taifa lenye miongo kadhaa tangu uhuru!
Umasikini tunaotakiwa kupigana nao kwa sasa,sio wa mali/pesa bali ni wa kukosa viongozi wenye maono (Vision) ambao ndio kimekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo ya taifa hili.
Adui mkubwa wa watanzania sasa sio Maradhi,umasikini na ujinga,kama alivyosema Mwl JK Nyerere, bali ni hao wapiga porojo wanaojiita viongozi/wanasiasa na hali uongozi hawaujui na hata hawajui siasa.
Tanzania sio masikini,kinachokosekana ni vipaumbele,hakuna hata siku moja,tukaweza kufanya vitu vyote kwa wakati mmoja,matokeo yake yatakuwa duni kwa sababu kutakuwa na divided attentions ambazo zitapelekea kupungua kwa ufanisi kwa kila kitu tunachogusa kufanya kama taifa,ambayo ni upotezaji wa rasili mali kama tunavyoona sasa!
Ukweli ni kwamba rasili mali kubwa kwa nchi yoyote ni watu,ndo maana nchi kama Canada na zingine za ulaya wanashawishi watu wahamie huko wapewe uraia ili watumike katika kujenga uchumi, je katika hili tanzania tutasema ni masikini na hali tuko 40milion. Rasili mali nyingine ni ardhi, je katika hili tutajitetea vipi? Kama kweli sio fikra mgando za hao wanaojiita viongozi wetu!
Aaaaaaaaagh! inaudhi bwana,hebu tufikirie kidogo nje ya box ili twende mbele. Sio lazima kuiga kila kitu kutoka nje ili kuendelea, wako wasomi watu hebu tuwatumie.
Viongozi wa tanzania wasikilizeni wananchi,na hasa hao wasomi na wenye uelewa,wanayo majibu sahihi ya matatizo yao/yetu. Na sio nyie kila kukicha mnajifungia kwenye vikao mkidhani mnaweza kuleta maendeleo ya tanzania kwa vikao na posho mnazojilipa! Na wala sio safari zenu za nje za kila siku ambazo kiukweli hazina faida kwa mtanzania wa kawaida.
Enyi viongozi,vueni hiyo miwani mlo vaa,manake mnakotupeleka kuna bonde kubwa,tutatumbukia humo na hatutapata wa kututoa,acheni kujifanya viziwi.
Ndimi Mkaapembeni!


No comments: