
Libya
Waasi wa Libya wanakimbia bandari ya mafuta ya Ras Lanuf baada ya mashambulio yaliyofanywa na majeshi yanayomtii Kanali Muammar Gaddafi.
Ripoti zinasema waasi walikuwa wakielekea na magari upande wa mashariki baada ya kushambuliwa na makombora.
Televisheni ya taifa ya Libya ilisema majeshi yanayomwuunga mkono Kanali Gaddafi pia yamewaondosha waasi kwenye bandari ya mafuta ya Sidra, magharibi mwa Ras Lanuf.
Katika siku za hivi karibuni, majeshi ya Kanali Gaddafi yamejaribu kudhibiti maeneo ya mashariki yaliyoshikiliwa na waasi, pamoja na mji wa Zawiya, magharibi mwa Tripoli.
Huko Ras Lanuf, muasi mmoja aliliambia shirika la habari la AFP: " Tumeshindwa. Wanarusha makombora na sisi tunakimbia. Hii inamaanisha wanadhibiti Ras Lanuf"
No comments:
Post a Comment