ANGALIA LIVE NEWS

Monday, May 23, 2011

JK achangia Sh10 mil Mfuko wa Elimu Nyamagana

Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Frederick Katulanda, Mwanza
RAIS Jakaya Kikwete, amefungua ukurasa mpya wa siasa za vyama vingi na maendeleo, kufutia kitendo chake cha  kumchangia Sh10 milioni, kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu katika Jimbo la Nyamagana, ambalo wananchi wake wanawakilishwa bungeni na mbunge kupitia tiketi ya Chadema.


Mchango wa Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa jimbo hilo linalowakilishwa na Ezekiel Wenje, umekuja wakati baadhi ya makada wa CCM wakiwa wamechangia kwa siri mfuko huo.Makada hao wamekuwa  wakitaka wasitajwe hadharani wakihofia kunyooshewa vidole kwa wameisaidia kambi ya upinzani.
Mgeni rasmi katika  harambee hiyo iliyofanyika juzi jijini Mwanza, Kabwe Zitto, alisema uamuzi wa rais kuchangia ulikuja baada ya yeye  kumpigia simu na kumuomba achangie.

Katika harambee hiyo iliyohudhuriwa na wageni mbalimbali, jumla ya Sh47 milioni, zilikusanywa na Zittoa kwa upande wake, alitoa  saaa yake ya mkononi ambayo ilinadiwa kwa Sh1.7 milioni.

Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema alikusanya kiasi kingine cha michango iliyowasilishwa kupitia njia ya mtando wa Facebook na ukurasa wake wa Twiteer.

Wengine waliochangia ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilibroad Slaa aliyechangia Sh5 milioni, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe Sh2 milioni na Wenje Sh3 milioni.Wabunge wa Chadema waliochangia kwa wakati huo  ni Grace Kiwelu aliyetoa Sh300,000, Muhonga Said Sh200,000 na Rayah Ibrahim Sh. 200,000.


Kwa upande wake, Naibu Meya wa Jiji la Mwanza, Charles Chinchibela alichangia Sh200,000 na wafanyabiashara mbalimbali wa Mwanza nao walitoa michango yao.

Akizungumza katika tuio hilo, Zitto aliwataka wanasiasa kuacha hulka ya kususia shughuli za maendeleo kwa vinsingizio vya itikati za kiasiasa na kwamba  siasa zinapaswa kutenganishwa na masuala ya maendeleo.

"Chama chochote kinaweza kuchangia maendeleo, lakini baadhi yetu wamekuwa waoga kwa visingizio vya kiasiasa, inasikitisha baadhi ya wanasiasa wanaogopa kuchangia maendeleo kwa kisingizio cha siasa, Rais Kikwete anapaswa kuwa mfano wa kuigwa na sisi wanasiasa kwa kuchangia maendeleo bila ubaguzi,"alisema Zitto.

CHANZO:MWANANCHI

No comments: