MKAZI wa Kijiji cha Nyaumata, Kata ya Somanda wilayani Bariadi, mkoani Shinyanga, Mayunga Mteremko ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kumuua mkewe.
Inadaiwa kwamba, Mteremko alimkatakata mapanga mkewe hadi kufa kutokana na wivu wa mapenzi.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha inasema, Mteremko anadaiwa kufanya tendo hilo baada ya kumuona mkewe, Kabula Lugiko (38) akiwa anasalimiana na Majaba Kimini (40).
Kamanda Kamugisha aliwaambia waandishi wa habari jana ofisini kwake kuwa mauaji hayo yalifanyika juzi saa 4 asubuhi katika Kijiji cha Nyaumata.
Kwa mujibu wa Kamanda, siku ya tukio Mteremko akiwa amejibanza karibu na shambani kwao alimuona Majaba akiwa anazungumza na mkewe wakati mwanamke huyo akiwa shambani.
Inadaiwa kwamba wanandoa hao walipokutana nyumbani, Mteremko alimhoji mkewe jambo alilokuwa akizungumza na Majaba hali iliyozusha mtafaruku.
“Kabula alikiri kuwa Majaba alikuwa akimtongoza lakini yeye hakukubali, kitendo kilichopingwa na mumewe Mteremko na kuamua kuchukua panga akaanza kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake mpaka kusababisha kifo chake papo hapo,” alisema Kamanda Kamugisha.
CHANZO:HABARI LEO
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake