Saturday, May 21, 2011

PAPARA NI CHANZO CHA WENGI KUFELI KITANDANI -GPL

Tumshukuru Mungu kwa kukutana tena leo. Family Radio inaendelea kusisitiza kwamba leo ndiyo mwisho wa dunia. Ni imani tu, lakini mimi naamini siku ya mwisho ni siri iliyopo kwa Mwenyezi Mungu pekee.

Hakuna mwingine anayejua. Hata malaika hawana ufahamu kuhusu siku hiyo. Wanajua dunia itafika mwisho lakini hawana utambuzi wowote kwamba itakuwa lini. Tungoje mwisho wa leo itakuwaje.


Turudi kwenye muktadha wetu. Papara ni sumu kubwa kwa mtu ambaye anahitaji kuwa mtendaji mzuri kwenye uwanja wa mapenzi. Wengi wameumbuka walipotaka kutekeleza hisia zao kwa nguvu kuliko uwezo wa mwili.

Nilieleza wiki iliyopita kuhusu Sued. Ni mfano hai ambao leo nitaeleza mwisho wake alipona vipi. Endapo wewe ni mwanaume ambaye umewahi kukabiliwa na tatizo kama lake basi moja kwa moja utapata tiba mahsusi.

 Si kwa mwanaume tu, nawe mwanamke una nafasi nzuri ya kusoma na kuelewa ili baadaye umsaidie mwenzi wako. Wakati mwingine inakuwa si papara ya mwanaume, bali anashindwa kwa sababu ya presha kutoka kwa mwenzi wake wa kike.

Mwanaume hushikwa na aibu inapotokea ameshindwa kutekeleza ipasavyo shughuli ya faragha. Lakini huumia zaidi pale anapoulizwa maswali yenye mrengo wa kusimangwa.

Mara nyingi wanawake huwanyanyapaa wanaume ambao hushindwa kumudu tendo na kuishia katikati, hiyo inasababisha wanaume wajitutumue kwa namna inayowezekana. Msongo wa mawazo huwasababishia ugonjwa wa kudumu.

Hivyo basi, wanawake wana nafasi nzuri ya kusoma na kuelewa ili waweze kutambua namna ya kuwasaidia wapenzi wao. Wasiwasimange, bali wawajenge kisaikolojia waondokane na papara wawapo faragha.

SUED ALIPONA VIPI?

Tatizo la Sued lilikuwa ni kurudi ulingoni mara ya pili. Hakujua kuwa mshindo mmoja unagharimu nishati nyingi, kwa hiyo hakusoma ubavu wake, hivyo akawa anajilazimisha kuunganisha. Hizo ndiyo papara ambazo hazitakiwi.

Hakutaka kuupa mwili nafasi ya kupumua baada ya mzunguko wa kwanza ili urejeshe nguvu. Akawa analazimisha, matokeo yake ‘jamaa’ akalala kabisa. Kila alipojitahidi kumwamsha akawa kama anamwambia alale zaidi. Aliteseka sana.

Sued alipokuja kuomba ushauri kwangu, kwanza nilimuuliza kazi yake. Akaniambia ni dereva wa daladala. Hapo ushauri wangu ukaanza mara moja. Niligundua kuwa anaporudi nyumbani anakuwa amechoka.

Pamoja na uchovu lakini hisia za ujana na mawazo potofu kuwa rijali ni lazima awe na uwezo wa kubadili wanawake na kurudia tendo mara nyingi, kwa maana pana ilikuwa ni sababu ya Sued kutaka tendo kwa pupa.

Nilipomshauri awe anatenga muda wa kuingia faragha, ajiamini mchezoni, afanye kwa uwezo na siyo kutaka 100 wakati uwezo wake ni 10 peke yake. Baada ya miezi mitatu alikuja na majibu kwamba yeye ni kidume che mbegu.

Hakika Sued hakuwa mgonjwa. Naomba niseme kwa kirefu namna ambavyo nilimpa tiba nikiamini kuwa inaweza kuwa suluhu ya matatizo ya wanaume wengi faragha. Ni muhimu pia kwa wanawake ili wawasaidie wenzi wao.

Itendelea wiki ijayo.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake