ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 24, 2011

SARATANI NI HATARI, UNAWEZA KUJIKINGA NAYO-GPL

Kansa ya mapafu.
Ni ukweli dhahiri kuwa ugonjwa wa saratani ni miongoni mwa magonjwa sugu na hatari yanayowasumbua watu wengi duniani. Idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa huu vinaongezeka kila siku.

Jitihada nyingi zinafanyika na taasisi na makampuni mbalimbali duniani ili kupambana na ugonjwa huu tishio. Mabilioni ya fedha hutumika kila mwaka duniani kote kutibu wagonjwa kwa njia mbalimbali, ikiwemo njia ya mionzi, vidonge, sindano, n.k.


Jitihada nyingi za taasisi hizo zimeelekezwa kwenye kutibu zaidi kuliko kuzuia na kujikuta kwenye lawama, hasa pale inapoonekana fedha nyingi zimekusanywa lakini vifo vingi bado vinaendelea na hakuna dalili ya kuushinda ugonjwa huu.

Nchini Marekani, kwa mfano, chama kinachopambana na magonjwa ya saratani, (American Cancer Society), katika kipidi cha mika 10 iliyopita, imekusanya zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 1.5 kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo, lakini wagonjwa wanaongezeka. Inaelezwa kuwa, idadi ya wagonjwa wanaokufa Marekani kutokana na saratani imeipita ile ya wale wanaokufa kwa magonjwa ya moyo.

HII INA MAANA GANI
Hali hii ina maana kwamba taasisi nyingi zimeshindwa kupambana na ugonjwa huu kwa sababu jitihada zao nyingi wamezielekeza kwenye kutibu zaidi kuliko kinga. Walitakiwa kutoa elimu na uelewa wa kutosha kuhusu chanzo cha magonjwa ya saratani. Uelewa mdogo wa aina ya vyakula tunavyotakiwa kula au kuacha, ndiyo chanzo kikuu cha ugonjwa huu.

Ugonjwa wa saratani ni wa kutengenezwa na binadamu mwenyewe, lakini kutokana na kukosekana kwa elimu ya kutosha kuhusu masuala ya lishe, watu hawajui vyakula vinavyosababisha  au vinavyozuia ugonjwa huu hatari.

Kwa upande mwingine, taasisi hizo zimeingia lawamani kwa kuwa zinaonekana kufurahia hali hii kwa sababu zinanufaika kiuchumi, kwa kuendelea kuuza dawa na mahitaji mengine yanayotakiwa na wagonjwa wa saratani.

Makampuni pamoja na taasisi hizo, hunufaika kwa kuwatibu au kuwasaidia wagonjwa wa saratani, hivyo watakosa fedha iwapo watu watajua njia za kujikinga na magonjwa hatari kama saratani. Kwa maana nyingine wao wamekaa kibiahara zaidi.

KINGA UNAYO MWENYEWE, INAWEZEKANA
Kinga kubwa dhidi ya ugonjwa wowote ule hususan saratani ni ulaji wa vyakula sahihi na kuepuka vyakula vyenye madhara mwilini. Vyakula vinavyoongoza kuwa chanzo cha saratani ni vile vilivyotayarishwa na kuwekwa kwenye makopo au makasha (Processed foods) ambavyo ndivyo vinavyoliwa kwa wingi hivi sasa duniani kote.

Pamoja na mambo mengine, ili kijiepusha na magonjwa hatari kama saratani, tumeshauriwa kupendelea kula vyakula halisi (organic food), hasa mboga za majani mbalimbamli na matunda ya aina mbalimbali na kubadili staili ya maisha yetu ya kila siku. Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia katika kujiepusha na saratani.

Dhibiti kiwango chako cha ‘insulin’ mwilini kwa kujiepusha na ulaji wa vyakula vya kusindika (processed food) pamoja na vyakula vyenye sukari nyingi. Wiki iliyopita tumeelezea kwa kirefu madhara yatokanayo na sukari.

Mwili lazima uwe na kiwango cha kutosha cha Vitamin D ambayo hupatikana kwa kuota jua la asubuhi. Vile vile pendelea kula samaki au virutubisho vyenye mafuta ya samaki aina ya Omega-3 kila siku ambavyo huimarisha afya ya moyo.

Fanya mazoezi ya kutosha mara kwa mara. Faida za mazoezi ni nyingi, ikiwemo ya kupunguza kiwango cha ‘insulin’ kama ilivyoelezwa hapo juu. Vile vile mazoezi yatakuwezesha kupunguza uzito ambao nao ukizidi huwa chanzo cha maradhi mengi.

Usingizi nao upo katika orodha ya vitu vya kuzingatia ili kujikinga na saratani, hakikisha unapata muda wa kutosha wa kulala. Jiepushe na mazingira yenye hewa kali za kemikali. Pendelea kula vyakula vya kuchemsha ua kuokwa zaidi kuliko vyakula vya kukaanga au kupikwa kwa mafuta mengi.

No comments: