ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, July 14, 2011

Marekani yaonya raia wake kwenda Sudan kusini-VOA

Wakazi wa Sudan kusini wakisheherekea uhuru wa taifa lao mjini Juba, Julai 9, 2011
Marekani inawaonya raia wake hatari ya kusafiri kuelekea Sudan Kusini  licha ya maadhimisho ya uhuru katika nchi hiyo mpya.

Ubalozi wa Marekani nchini Sudan kusini uliwasihi wamarekani Jumanne kutosafiri kuelekea mikoa  ya mpakani  kati ya Sudan na Sudan kusini  ikielezea mapigano ya karibuni kati ya majeshi yanayotii wakuu wa  nchi hizo mbili pamoja na kuongezeka kwa majeshi pande zote za mpaka.


Ubalozi unasema ukiongezea  mapigano hayo ya ardhini, jeshi la anga la Sudan limepiga maeneo ya mpaka katika majimbo ya Unity na Kordofan kusini. Ubalozi pia umeonya hatari ya ghasia katika maeneo yote ya Sudan kusini  ikisema kuna majeshi tofauti ya  waasi  yasiyopungua saba ambayo mara kwa mara yanapambana na majeshi ya Sudan kusini.
Ubalozi unasema serikali ya Sudan kusini ina uwezo kiasi wa kupambama na uhalifu nje ya mji mkuu wa Juba na kwamba hata hapo walipo  hatari ya ghasia za uhalifu zipo juu. 
Sudan kusini imekuwa taifa jipya siku ya Jumamosi baada ya wakazi wake walipopiga kura kwa wingi kujitenga kutoka kaskazini katika kura ya maoni ya mwezi Januari. 

Sudan ilipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka 21 ambavyo vilimalizika mwaka 2005. Sudan na Sudan kusini bado wana mizozo kadhaa ambayo haijatatuliwa ikiwemo nani atadhibiti mkoa wa Abyei wenye utajiri wa mafuta na namna ya kushirikiana katika mapato ya mafuta. 

No comments: