ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 20, 2011

Polisi adakwa akimtorosha majeruhi wa risasi wodini

Jeshi la Polisi mkoani hapa, limeingia katika tuhuma nzito kwa madai ya askari wake kutaka kumtorosha wodini kijana aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi kwa lengo la kutaka kumsaidia mfanyabiashara ambaye kutenda kosa hilo kutoka rumande.
Tukio la kutaka kutoroshwa majeruhi huyo lilitokea julai 17 mwaka huu majira ya mchana katika wodi namba moja ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.

Inadaiwa kuwa askari huyo anadaiwa kutumwa na mfanyabiashara kumtorosha majeruhi huyo, Abisai Joseph (25) mkazi wa Kihonda Manispaa ya Morogoro katika Wodi namba 1 ya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro ambako amelazwa kwa matibabu.
Tukio hilo limetokea siku mbili baada ya Abisai kupigwa risasi katika mguu wake wa kulia na mfanyabiashara huyo wa Mkoa wa Arusha na Morogorokatika ukumbi wa disko wa Four Stars mjini Morogoro Julai 15, mwaka huu usiku.
Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni mfanyabiashara huyo kutaka kumgonga na gari Abisai nje ya ukumbi huo na alipohoji ndipo akafyatua risasi hewani na kumchapa mguuni.
Ndugu na marafiki wa Abisai walidai baada ya kupigwa risasi na kulazwa, jumapili iliyopita askafri huyo a mmoja wa askari alifika katika wodi hiyo na kumrubuni ili atoke bila ruksa ya daktari kwa ahadi kuwa mtuhumiwa aliyempiga risasi alikuwa ameahidi kumlipa fidia na kugharamia matibabu.
Ndugu hao walisema askari huyo alifanikiwa kumrubuni mgonjwa wao na walipoanza kutoka wodini hapo walimrudisha mlangoni na kumpiga marufuku kuzungumza na askari yeyote yule na kumuwekea ulinzi
Kijana huyo alithibitisha kufuatwa na kurubuniwa na askari huyo ili waweze kufuta tuhuma dhidi ya mfanyabiashara huyo Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk. Baraka Nzobo alisema hakukuwa na ruksa iliyokuwa imetolewa kwa majeruhi huyo jumapili iliyopita kwa kuwa alikuwa bado anatakiwa kupewa matibabu na kuchukuliwa vipimo zaidi.
Kaimu kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Joseph Rugila, alisema hana taarifa na tukio la kijana huyo kujeruhiwa kwa kupigwa risasi na hata alipoomba taarifa ya matukio ya wiki nzima iliyopita kwa wasaidizi wake halikuwamo kwenye orodha. Kaimu kamanda huyo aliwaita ofisini kwake mkuu wa polisi wa wilaya ya Morogoro Mjini John Laswai, na Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya hiyo, Brack Magesa na kuwahoji sababu za kutompa taarifa juu ya tukio hilo.
Kwa pamoja walidai kuwa hilo lilikuwa moja kati ya matukio madogo hivyo hawakuona haja ya kuripotiwa hatua ambayo ilimfanya Rugila kuhoji udogo wa wake huku likiwa limehusisha kujeruhi kwa bastora.
CHANZO: NIPASHE

No comments: