ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 13, 2011

SHUKURANI ZA DHATI.KWA .MAFANIKIO.N.E UMOJA 2011


Ndugu wanajumuia.....
Kwa niaba yangu binafsi,na hasa kwa niaba ya wanakamati wenzangu,ningependa kutoa shukurani zangu za dhati kwenu nyote mliochangia,mlioshughulika, na hasa kwa kuhudhuria kwenu na kufanikisha tena shughuli yetu ya mwaka huu. Bila upendo na moyo wenu wa kujitolea, shughuli hii isingefanikiwa.

Baada ya uchovu wa tangu jumapili, kuanza kupungua, nimeona ni muhimu kama ada, kutoa shukurani zangu za dhati, kwa yale yote mazuri yaliyotendeka. Kwa upande wa Mpira wa miguu tunawapongeza sana ndugu zetu wa
West  kwa kuchukuwa kikombe,na kutimiza ahadi yao waliyoitowa kuwa wao sio "Maharage ya mbeya" na wamesema always there will be next year..... Kushney Kushney Kushney!!!
Shukurani kwa wakina mama wote waliojishughulisha kwa kila jambo, hasa hasa kwa Mnuso wa Mahanjumati yalikuwa sio mchezo. Asante sana kwa vijana wa Springfield kwa maandalizi ya nyama na uwanja,Shukurani kwa waliotuchomea nyama pale jikoni, Mungu awabariki wote.  Wale  wote walioshiriki kwenye maonyesho ya mavazi chini ya usimamizi wa Edna Eliamani na gwiji wa Mitindo Asya Idarous, tamasha la mavazi la mwaka huu Iilikuwa kabambe na lakuvutia sana!.
Napenda kutoa shukurani zangu za dhati Kwa Nene na kikundi chake cha ngoma  ya asili, na vilevile shukurani za zati zimuende Mwenyekiti wa California Bwana Iddi Mtango na Dada yetu Agness Mosses, kwa kuja kwao kwani kumetuelimisha na Mengi.

Napenda pia kutoa shukurani zangu za dhati kwa "Master's of ceremony" kwa kazi nzuri  ya kuifanikisha shughuli yetu. Shukurani za pekee tunazitoa kwa bwana Hasheem Thabeet, kwa mchango wake wa hali na mali, na hasa kwa kuamua kuja kuungana nasi katika shughuli hii ya kijumuia. Tunamshukuru pia kwa upendo wake aliouonyesha kwa vijana wadogo wengi waliokuja na kufurahi pamoja nae katika mchezo wa mpira wa kikapu. Vijana walifurahi sana, na tunakukaribisha tena mwakani mwakwetu. Kwa niaba ya New England Umoja, , tunakutakia mafanikio mema katika msimu ujao wa N.B.A, na timu yako mpya ya Houston Rockets!.
Shukurani kwa kila mmoja wenu, aliefanya kila juhudi ya kuifanya shughuli hii iendelee kuwa na vivutio tofauti kila mwaka. Asanteni wageni wote mliokuja kutoka sehemu mbalimbali hapa Marekani, Mungu awabariki wote pia na nchi yetu nzuri ya Tanzania. Mungu akipenda Panapo majaaliwa tukutane tena. Usije ukakosa uhondo,kwani itakuwa ni shughuli ya aina yake tena 2012!!.
Tumuombe Mungu Atupe Uhai na afya njema.
Tutakuwa na Mkutano wa kufunga mwaka ili kuchambua shughuli yote ilivyokwenda, yakiwemo mapato na matumizi ya fedha ya shughuli ya mwaka huu, hali ya chama kwa ujumla, na maandalizi ya mkutano mkuu wa wanachama na uchaguzi wa viongozi kwa muda mwingine wa miaka miwili. Hizo ni baadhi ya ajenda zitakazojadiliwa katika kikao cha wanakamati september 4th, Nitawajuulisheni Mahali utakapo fanyika mkutano huo
Asanteni sana.

No comments: